Pata taarifa kuu

Urusi na Marekani wabadilishana wafungwa, Griner na muuza silaha Bout waachiliwa

Urusi imemuachilia huru mchezaji wa mchezo wa kikapu Brittney Griner, baada ya kubadilishana na mfungwa mwingine, raia wa Urusi Viktor Bout, mfanyabiashara wa silaha aliyekuwa anashikiliwa nchini Marekani. Hili limewezeshwa na nchi ya Falme za Kiarabu. 

Nyota wa WNBA na mshindi wa medali ya dhahabu mara mbili ya Olimpiki Brittney Griner akiwa kizimbani akisikiliza uamuzi wa mahakama akiwa amesimama katikachumba cha mahakama huko Khimki, nje kidogo ya Moscow, Urusi, Alhamisi, Agosti 4, 2022.
Nyota wa WNBA na mshindi wa medali ya dhahabu mara mbili ya Olimpiki Brittney Griner akiwa kizimbani akisikiliza uamuzi wa mahakama akiwa amesimama katikachumba cha mahakama huko Khimki, nje kidogo ya Moscow, Urusi, Alhamisi, Agosti 4, 2022. © Evgenia Novozhenina / AP
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa Urusi na Marekani wamesema Griner ameachiwa katika hatua ya ngazi ya juu ya ubadilishanaji wa wafungwa.

Griner ni bingwa mara mbili wa Olimpiki na timu ya taifa ya wanawake ya Marekani.

Griner alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Moscow mwezi Februari kwa kumiliki mafuta ya bangi na mwezi uliopita alipelekwa kwenye mahakama ya adhabu.

Naye Viktor Bout alipokamatwa katika hoteli moja katika mji mkuu wa Thailand Bangkok mwaka 2008, hatua ilioikasirisha serikali ya Urusi.

Aliuza silaha kwa wababe wa vita na serikali, na kuwa mmoja wa watu wanaosakwa sana duniani.

Utawala wa Biden ulikuwa umependekeza kubadilishana wafungwa, ikifahamu kwamba Moscow ilikuwa ikitaka kuachiliwa kwa Bout kwa muda mrefu.

Ubadilishanaji huo wa wafungwa umefanyika huko Abu Dhabi na umefanyika wakati wa mivutano mikubwa iliyoko kati ya Marekani na Urusi kuhusiana na vita vya Ukraine. Makubaliano haya ya kubadilishana wafungwa ambayo ni ya pili kufanyika katika kipindi cha miezi 8 kati ya nchi hizi mbili, yamepelekea kuachiwa kwa mtu maarufu zaidi raia wa Marekani aliyekuwa amefungwa nje ya nchi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.