Pata taarifa kuu
MAREKANI-USALAMA

Joe Biden azitembelea familia za wahanga wa shambulizi la bunduki Uvalde

Rais wa Marekani Joe Biden ametembelea familia za wanafunzi 19 na walimu wawili, waliouawa kwa  kupigwa risasi wakiwa shuleni wiki iliyopita katika mji wa Uvalde, jimboni Texas.

Joe Biden na mkewe Jill wakitoa heshima zao nje ya ukumbusho wa shule ya Msingi ya Robb mnamo Mei 29, 2022.
Joe Biden na mkewe Jill wakitoa heshima zao nje ya ukumbusho wa shule ya Msingi ya Robb mnamo Mei 29, 2022. AP - Evan Vucci
Matangazo ya kibiashara

Biden na mkewe walibubujikwa machozi walipofika eneo la kumbukumbu ya wahanga ambako kuna picha za wanafunzi na walimu waliouwawa pamoja rundo la mashada ya maua na kadi zenye salamu nyingi za rambirambi kutoka kwa watu walioguswa na mkasa huo.

Wakiwa wamevalia mavazi meusi yanayoashiria maombolezo, rais Biden na mkewe walitembea taratibu kutazama picha ya kila aliyepoteza maisha wakati wa shambulizi la wiki iliyopita ambalo linatajwa kuwa baya zaidi kuwahi kutokea nchini Marekani kwa karibu muongo mmoja.

Naye Makamu wa rais Kamala Harris, amesema wakati umefika wa kusitsiha matumizi mabaya ya bunduki nchini humo.

Wakati huo huo, idara ya haki imesema itachunguza namna polisi walivyoshughulikia tukio hilo ambalo limezua hasira nchini Marekani, kuhusu kuendelea kwa matukio ya watu kupigwa risasi mara kwa mara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.