Pata taarifa kuu

Jumuiya ya kimataifa yakusanya dola milioni 600 kusaidia Haiti

Jumatano huko Port-au-Prince, wafadhili wa kimataifa waliahidi kutoa dola milioni 600 kusaidia kujenga tena kusini mwa Haiti. Zaidi ya miezi sita iliyopita, mnamo Agosti 14, eneo hilo liliharibiwa na tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 7.2 katika vipimo vya Richter ambalo liliua zaidi ya watu 2,200 na kuharibu zaidi ya nyumba 130,000.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed katika mkutano na waandishi wa habari mjini New York Septemba 2020.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed katika mkutano na waandishi wa habari mjini New York Septemba 2020. AFP - ESKINDER DEBEBE
Matangazo ya kibiashara

Dola bilioni mbili katika kipindi cha miaka minne: hizi ni pesa zinazohitajika kwa ujenzi wa kusini mwa Haiti. Milioni 600 iliyoahidiwa Jumatano hii, Februari 16 inaweza isionekane kuwa nyingi, lakini ni kubwa kuliko matarajio ya awali ya Umoja wa Mtaifa. Amina Mohammed, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, hasa alikaribisha mtazamo mpya kati ya wafadhili wa kimataifa na Haiti, ambao ulifafanua vipaumbele vya mpango wa ujenzi mpya.

"Michango hii, mikubwa na midogo, inadhihirisha kwamba jumuiya ya kimataifa imejitolea katika mbinu mpya ya kufanya kazi na serikali na raia wa nchi hii," alisema.

Wafadhili wa kigeni na serikali ya Haiti kwa hivyo wanataka kuhakikisha kwamba mafunzo yamepatikana kutokana na makosa ya siku za nyuma, hasa usimamizi wa mkanganyiko na usioratibiwa wa misaada baada ya tetemeko la ardhi la Januari 2010.

Pesa zilizoahidiwa zitawekwa katika hazina iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa na kusimamiwa na mashirika kadhaa ya kitaifa na yale ya kigeni. Ariel Henry, Waziri Mkuu wa Haiti, amehakikishia kuwa pesa hizo zitatumika kama ilivyopangwa. "Tunaahidi kila mtu, wafadhili wote kwamba pesa hizi zitatumika vizuri, kwa uwazi, kwa kuwahudumia wakazi wa kusini mwa kina," amesema.

Hata hivyo Amina Mohammed alikumbusha uzito wa mzozo wa kijamii na kiuchumi unaoikumba Haiti kwa sasa: karibu wakaazi milioni tano kati ya milioni kumi na moja wa kisiwa hicho bado wanahitaji msaada wa kibinadamu mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.