Pata taarifa kuu

Somalia: Washington yatishia kuchukuwa vikwazo ikiwa kalenda ya uchaguzi haitaheshimiwa

Marekani inatishia kuweka vikwazo dhidi ya mtu yeyote ambaye atahujumu kalenda mpya ya uchaguzi nchini Somalia iliyotangazwa wikendi hii.

Wanajeshi wanaomuunga mkono Sadaq Omar Hassan huko Mogadishu.
Wanajeshi wanaomuunga mkono Sadaq Omar Hassan huko Mogadishu. © REUTERS - FEISAL OMAR
Matangazo ya kibiashara

Jumapili jioni, na baada ya kuahirishwa mara kadhaa, Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble na wakuu wa majimbo mbalimbali ya Somalia wameahidi kukamilisha uchaguzi wa wabunge kabla ya Februari 25, hatua muhimu kabla ya uchaguzi wa urais. Lakini ahadi hii imepokelewa kwa tahadhari na kwa mashaka.

Umoja wa Mataifa umejizuia kuzungumzia chochote kuhusiana na ahadi hii ya waziri mkuu wa Somalia. Umoja wa Mataifa ulikubali makubaliano hayo siku ya Jumatatu, lakini mara moja uliwataka viongozi wa Somalia "kuepuka uchochezi unaoweza kuleta mvutano mpya" na "kuendelea kushikamana kuhusiana na kuwekwa kwa haraka mchakato wa uchaguzi unaoaminika". Marekani inakwenda mbali zaidi, ikiashiria tishio la kuchukuwa vikwazo.

"Tunatoa wito kwa viongozi wote wa Somalia, kitaifa na kishirikisho, kuheshimu ratiba mpya na kukosoa makosa ya kiutaratibu ambayo yameathiri mchakato huo hadi sasa," amesisitiza Ned Price, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. Uchaguzi nchini Somalia umechelewa kwa zaidi ya mwaka mmoja, na Februari 8 itakuwa ni mwaka mmoja tangu muhula wa rais kuisha. Marekani iko tayari kutumia zana zinazofaa, ikiwezekana ikiwa ni pamoja na vizuizi vya viza, kujibu ucheleweshaji zaidi au hatua zinazoathiri uadilifu wa mchakato wa uchaguzi. "

Wachambuzi kadhaa pia wanaelezea mashaka yao. Kulingana na kalenda hiyo mpya, zimesalia siku 45 nchini Somalia kuhitimisha mchakato tata wa uchaguzi, na hasa uliohujumiwa na mizozo ya kisiasa na kiukoo. Isitoshe mgogoro kati ya rais na waziri mkuu kuhusu muundo wa kamati inayohusika na migogoro ya uchaguzi haujatatuliwa kikamilifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.