Pata taarifa kuu
MAREKANI

Marekani kumshtaki muaji wa Daniel Pearl

Marekani inajaribu kumfungulia mashitaka mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya Daniel Pearl kwa vyomba vya sheria vya nchi hiyo baada ya mahakama ya Pakistani wiki iliyopita kuamuru kuachiliwa mara moja kwa watu wanne wanaotuhumiwa kumteka nyara na kumuua mwandishi huyo wa habari wa Marekani.

Mwanahabari wa Marekani Daniel Pearl
Mwanahabari wa Marekani Daniel Pearl MARK RALSTON / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ahmed Omar Saïd, mshukiwa mkuu katika kesi hii, alijikuta hukumu ya kifo dhidi yake mwezi Aprili mwaka jana ikipunguzwa na kuhukumiwa kifungo cha miaka saba jela, wakati washukiwa wengine watatu waliachiwa huru.

"Maamuzi tofauti yaliyotengua hatia yake na kuagiza aachiliwe ni dharau kwa waathiriwa wa ugaidi ulimwenguni kote," amesema Kaimu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Marekani.

Ikiwa hatua za kurudisha hatia ya Saïd hazitafanikiwa, Marekani "iko tayari" kumtia kizuizini na kumfikisha mahakamani, ameongeza Jeffrey Rosen katika taarifa.

"Hatuwezi kumruhusu kutoroka haki kwa kuhusika kwake katika utekaji nyara na mauaji ya Daniel Pearl," aamebaini Jeffrey Rose.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.