Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFYA-COVID 19

Covid-19 Marekani: Biden aahidi chanjo milioni 100 katika siku 100 za kwanza katika muhula wake

Rais mteule wa Marekani Joe Biden ametangaza timu yake itakayohusika na mapambano dhidi ya janga la COVID-19, ikiwa ni pamoja na Waziri wake mpya wa Afya, Xavier Becerra, mwanasheria mkuu wa sasa wa California.

Rais mteule wa Marekani Joe Biden
Rais mteule wa Marekani Joe Biden Angela Weiss / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuapishwa kuwa rais rasmi wa Marekani Januari 20, Joe Biden anataka kuifanya COVID-19 kuwa kipaumbele chake na atangaza mpango wa mapambano kwa siku 100 za kwanza za muhula wake.

Kutoka ngome yake ya Wilmington, Joe Biden ametangaza mpango wake wa kupambana na ugonjwa hatari wa COVID-19 pamoja na malengo matatu rahisi sana: barakoa, chanjo na kufunguliwa kwa shule katika siku 100 za kwanza za muhula wake.

"Tutavaa barakoa kila sehemu zote ambapo inawezekana," amesema Joe Biden. Barakoa kwa sote katika kipindi cha siku 100 za kwanza katika muhula wangu. Hili ni jambo rahisi mnaloweza kufanya kupunguza idadi ya visa vya maambukizi ya COVID-19. "

Katika siku zake 100 za kwanza za muhula wake, Joe Biden pia anataka nchi yake kutumia chanjo milioni 100: “Hii itakuwa kampeni ya chanjo yenye ufanisi zaidi katika historia ya Marekani,  " ameongeza rais mteule wa Marekani

Kwa kukabiliana na COVID-19, rais mteule anawategemea watu wawili: Xavier Becerra, Waziri wake mtarajiwa wa Afya na Daktari Anthony Fauci anayeheshimiwa sana, ambaye tayari anasimamia kitengo kinacho kabiliana na mgogoro wa kiafya katika Ikulu ya White House, ambaye amepoteza aimani kwa Donald Trump . "Lazima tutawale na sayansi," amesema mtaalam wa kinga.

Wakati huo huo katika Ikulu ya White House, Donald Trump pia amefanya mkutano kuhusu Corona, lakini hakuna mjumbe wa timu ya Biden aliyealikwa. Na wakati mwandishi wa habari alipouliza ni kwanini wahjumbe hao hawajaalikwa katika mkutano huo, "Tutaona utawala unaofuata utakuwa aje, natumai utakuwa utawala wa Trump," amejibu rais anayemaliza muda wake, ambaye bado anaendelea kukana kuwa alishindwa katika uchaguzi wa urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.