Pata taarifa kuu
MAREKANI-SIASA

Marekani: Jenerali mstaafu mweusi kuteuliwa kuongoza Pentagon

Rais mteule wa Marekani Joe Biden anatarajia kumteua Jenerali mstaafu mweusi kuwa mkuu wa makao makuu ya jeshi la Marekani, Pentagon.

Joe Biden, rais mteule wa Marekani
Joe Biden, rais mteule wa Marekani AP Photo/Andrew Harnik
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo bado sio rasmi lakini kulingana na vyombo vya habari vya Marekani, Joe Biden ameamua kumteua Jenerali mstaafu Lloyd Austin kuwa Waziri wa Ulinzi.

Lloyd Austin atakuwa Mmarekani mweusi wa kwanza kuongoza Pentagon. Tangazo hilo linaweza kutolewa leo Jumanne.

Kizuizi cha kwanza cha Llyod Austin kuthibitishwa kuwa Waziri wa Ulinzi haitakuwa rangi yake ya ngozi, lakini kwa kushangaza ni kazi yake ya kijeshi ya muda mrefu. 

Bunge la Marekani limekuwa likisisitiza juu ya uteuzi wa raia kuchukuwa nafasi ya kuliongoza jeshi la nchi hiyo.

Hapo awali, uteuzi wa wanajeshi wawili ambao walikuwa bado kazini ulikubaliwa. Kama wanajeshi hao, Lloyd Austin anatarajia ridhaa ya wabunge ili aweze kudhibitishwa.

Jenerali huyu wa nyota 4, aliyestaafu tangu mwaka 2016, ataingia kwenye historia kwa kuwa Waziri wa Ulinzi wa kwanza kutoka jamii ya Wamarekani weusi. Kulingana na vyombo vya habari vya Marekani, Joe Biden alimpendekezea kazi hiyo siku ya Jumamosi na Jenerali Austin alikubali mara moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.