Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFYA-COVID 19

Wakili wa Donald Trump, Rudy Giuliani, apatikana na virusi vya Corona

Rais wa Marekani Donald Trump, kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa wakili wake, Rudy Giuliani ambaye aliwahi kuhudumu kama meya wa jimbo la New York, amepatikana na virusi vya corona.

Rudy Giuliani, wakili wa rais wa Marekani Donald Trump
Rudy Giuliani, wakili wa rais wa Marekani Donald Trump Angela Weiss / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika ujumbe wake kwenye ukurasa wake wa Twitter, rais Trump amemtakia Giuliani nafuu ya haraka, huku akipongeza juhudi zake zujaribu kufichua ufisadi katika uchaguzi mkuu uliopita wa Novemba 3.

Giuliani mwenye umri wa miaka 76 na ambaye amekuwa akiongoza kampeni ya rais Trump ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa Novemba 3 katika baadhi ya majimbo anakuwa mshirika wa karibu wa rais Trump wa hivi punde kuambukizwa virusi vya Corona

Hapo jana mratibu wa kikosi kazi cha ikulu ya White House kinachochugulikia janga la corona Dr Deborah Birx, alikosoa utawala wa Trump kwa kukiuka malekezo ya kujikinga na kuendeleza taarifa za uongo kuhusu janga la Corona.

Hadi kufikia sasa, zaidi ya Wamarekani Milioni 14.6 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona, huku Wamarekani zaidi ya laki mbili na elfu themanini wakifariki kutokana na virusi hivyo, kwa mujibu wa takwimu za kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Johns Hopekins.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.