Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA-MADURO

Kambi ya Maduro yashinda uchaguzi wa wabunge uliosusiwa na upinzani

Tume ya uchaguzi nchini Venezuela imetangaza Jumatatu kwamba wagombea wanaomuunga mkono rais Nicolas Maduro wamehakikishiwa kwamba wataendelea kudhibiti bunge kufuatia uchaguzi wa wabunge uliosusiwa na vvyama vya upinzani.

Rais wa Venezuela  Nicolas Maduro
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro REUTERS/Manaure Quintero
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kwenye runinga, mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi, Indira Alfonzo, amebaini kwamba kambi ya Maduro imeshinda 67.6% ya kura milioni 5.2 zilizopigwa. Ni 31% tu ya wapiga kura waliojiandikisha ambao walishiriki katika zoezi la kupiga kura.

Upinzani, ambao ulikuwa na viti vingi katika Bunge lililomaliza muda wake, ulitoa wito wa kususia uchaguzi huo, wakilaani uchaguzi 'usiofaa'.

"Matokeo yatayotangazwa na utawala haramu wa Maduro hayaendani na matakwa ya wananchi wa Venezuela,"

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo alisema Jumapili. "Kinachotokea leo ni udanganyifu, sio uchaguzi," aliaongeza kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Juan Guaido, ambaye aliongoza Bunge linalomaliza muda wake, alitambuliwa na zaidi ya nchi 50, ikiwa ni pamoja na Marekani, kama rais halali wa mpito wa Venezuela, kufuatia kuchaguliwa tena kwa Nicolas Maduro mnamo mwaka 2018 katika mazingira ambayo yalionekana sio halali na mataifa mengi ya magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.