Pata taarifa kuu
MAREANI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Marekani 2020: Trump aombwa kukubali matokeo ya uchaguzi yanayompa ushindi Joe Biden

Mshirika wa karibu wa rais Donald Trump, ambaye pia aliwahi kuwa gavana wa jimbo la New Jersey Chris Christie, amemtaka Trump kukubali matokeo ya uchaguzi uliompa ushindi mpinzani wake wa karibu Joe Biden.

C’est la première fois que Donald Trump s’exprime publiquement depuis que la victoire de Joe Biden à la présidentielle a été annoncée. Il s’est uniquement exprimé sur la pandémie de coronavirus qui bat des records en ce moment aux États-Unis.
C’est la première fois que Donald Trump s’exprime publiquement depuis que la victoire de Joe Biden à la présidentielle a été annoncée. Il s’est uniquement exprimé sur la pandémie de coronavirus qui bat des records en ce moment aux États-Unis. MANDEL NGAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika matamshi yake, Chris Christie, ametaja kikosi kinachomshauri Trump kwa masuala ya kisheria kama aibu kwa taifa.

Rais Trump, amekataa kubali kushindwa, kwa madai kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na dosari, madai ambayo hadi sasa ameshindwa kueleza yalivyofanyika.

Wengi wa wajumbe wa chama cha Republican, wameonekana kuunga mkono madai yake Trump,  huku baadhi yao wakionekana kuwa na msimamo tafauti na ule wa chama.

Siku ya Jumamosi, Donald Trump alipata pigo katika azima yake ya kupinga matokeo ya eneo la Pennsylvania, baaada ya jaji kutupilia mbali kesi ya madai ya wizi wa kura baada ya kuhesabiwa upya.

Kutokana na agizo hilo la mahakama, hii leo ,eneo la Pennsylvania ,linatarajiwa kumtangaza rais mteule Joe Biden Kutoka chama cha Democratic, kama mshindi kwa kupata kura zaidi ya 80,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.