Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Edison Research: Biden afikisha wajumbe maalumu 243 dhidi ya 214 wa Trump

Mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden anaendelea kufanya vizuri katika majimbo mabalimbali nchini Marekani wakati tayari amefikisha wajumbe 243 idhidi ya 214 wa rais Donald Trump, kulingana na makadirio ya hivi karibuni ya shirika la Edison Research.

Joe Biden na Donald Trump,Septemba 29, 2020, wakati wa mdahalo wa kwanza wa televisheni kabla ya uchaguzi wa urais, Novemba 3, 2020.
Joe Biden na Donald Trump,Septemba 29, 2020, wakati wa mdahalo wa kwanza wa televisheni kabla ya uchaguzi wa urais, Novemba 3, 2020. JIM WATSON, SAUL LOEB / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani huchaguliwa na kundi la wajumbe 538 ambao huamua mshindi.

Mfumo wa Uchaguzi wa Marekani kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, umewapa mamlaka wajumbe hao kumchagua mshindi.

Waliaondika Katiba ya Marekani waliamua kuwe na wajumbe hawa kwa hofu kuwa huenda, wapiga kura wasifanye maamuzi sahihi lakini pia ilihofiwa kuwa majimbo yenye idadi kubwa ya watu wangekuwa na nafasi kubwa ya kuamua mshindi wa uchaguzi nchini humo.

Kila jimbo nchini Marekani angalau lina wajumbe watatu, lakini jimbo la Califonia ambalo ndilo lenye watu wengi nchini Marekani lina wajumbe 55, huku Texas likiwa na wajumbe 38.

Ili kuibuka mshindi, mgombea anastahili kupata angalau kura 270 za wajumbe hao.

Majimbo ambapo Donald Trump aliibuka msindi

Alabama, Arkansas, South Carolina, North Dakota, South Dakota, Florida, Idaho, Indiana, Iowa, Kansas, Kentucky, Louisiana, Maine (1) Mississippi, Missouri, Montana, Nebraska (wajumbe maalumu4), Ohio, Oklahoma , Tennessee, Texas, Utah, West Virginia na Wyoming.

Majimbo ambapo Joe Biden ameshinda

California, Colorado, Connecticut, Delaware, Wilaya ya Columbia (Washington), Hawaii, Illinois, Maine (3) Maryland, Massachusetts, Michigan, Minnesota, Nebraska (mjumbe maalumu 1), New Hampshire, New Jersey, New Mexico, New York , Oregon, Rhode Island, Vermont, Virginia na Jimbo la Washington.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.