Pata taarifa kuu
MAREKANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Marekani kuchukua hatua kali kukabiliana na maambukizi mapya

Kitengo kinachokabiliana na mgogoro wa kiafya unaosababishwa na virusi vya Corona katika ikulu ya White House kimetaka hatua kali zichukuliwe wakati idadi ya maambukizi ilifikia kiwango cha juu siku ya Alhamisi.

atika ngazi ya kitaifa, maafisa wa afya walithibitisha siku ya Alhamisi kuwa watu wengine 91,248 wamepatikana wameambukizwa virusi vya COVID-19 katika muda wa saa 24 zilizopita, ongezeko kubwa zaidi kwa siku moja kulingana na REUTERS.
atika ngazi ya kitaifa, maafisa wa afya walithibitisha siku ya Alhamisi kuwa watu wengine 91,248 wamepatikana wameambukizwa virusi vya COVID-19 katika muda wa saa 24 zilizopita, ongezeko kubwa zaidi kwa siku moja kulingana na REUTERS. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya visa vipya 91,000 vimethibitishwa katika muda wa saa 24 zilizopita nchini Marekani.

Mikoa iliyoathirika zaidi inapatikana Magharibi mwa nchi na Midwest na inajumuisha majimbo muhimu yanayotarajiwa kuchukua jukumu kubwa katika uchaguzi wa urais wa Jumanne.

"Tuko kwenye njia ngumu. Tunaenda katika njia isiyofaa," amesema Dk Anthony Fauci wa kitengo cha mgogoro kilichowekwa kupambana na janga la COVID-19.

Daktari Anthony Fauci, mmoja wa maafisa wa juu wa magonjwa ya kuambukiza nchini Marekani, amesema visa vya ugonjwa wa COVID-19 vinaongezeka katika majimbo 47.

Katika ngazi ya kitaifa, maafisa wa afya walithibitisha siku ya Alhamisi kuwa watu wengine 91,248 wamepatikana wameambukizwa virusi vya COVID-19 katika muda wa saa 24 zilizopita, ongezeko kubwa zaidi kwa siku moja kulingana na takwimu za shirika la habari la REUTERS.

Zaidi ya watu 229,000 wamefariki dunia kutokana na COVID-19 nchini Marekani na nchi hiyo ina maambukizi karibu milioni 9 hadi sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.