Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-CORONA-AFYA

Donald Trump apatikana na virusi vya Corona

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza mapema asubuhi leo Ijumaa, Oktoba 2, kwamba amepimwa na kupatikana na virusi vya Corona, pamoja na mkewe Melania.

Kulingana na daktari wa Ikulu ya White House, Donald Trump na mkewe "wote wanaendelea vizuri na wanapanga kubaki Ikulu wakati huu wanapoendelea kufuata maelekezo ya madaktari."
Kulingana na daktari wa Ikulu ya White House, Donald Trump na mkewe "wote wanaendelea vizuri na wanapanga kubaki Ikulu wakati huu wanapoendelea kufuata maelekezo ya madaktari." REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Donald Trump, ambaye anawania muhula wa pili katika uchaguzi wa urais wa Novemba 3, alisema siku ya Alhamisi kwamba amejiweka karantini baada ya mmoja wa washauri wake wa karibu, Hope Hicks, kupatikana na virusi vya Corona.

"Usiku wa leo @FLOTUS (Mke wa rais wa Marekani) na mimi tumeatikana na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19. Tumeanza kujiweka karantini na kuanza kufuata utaratibu unaotolewa na madaktari, " amesema rais wa Marekani kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Kulingana na daktari wa Ikulu ya White House, Donald Trump na mkewe "wote wanaendelea vizuri na wanapanga kubaki Ikulu wakati huu wanapoendelea kufuata maelekezo ya madaktari." Rais wa Marekani "ataendelea na majukumu yake", ameongeza daktari wake.

Ikulu ya White House imetangaza kufutwa kwa ziara ya rais Donald Trump katika Jimbo la Florida, ziara iliyokuwa imepangwa leo Ijumaa kwa mkutano wa kampeni zikisalia siku chache kabla ya uchaguzi wa urais wa Novemba 3.

Awali Donald Trump alikuwa amethibitisha kuwa Hope Hicks, mshauri wake wa karibu, alipatikana na ugonjwa huo hatari. Alikuwa na rais wa Marekani katika ndege ya Force One, aliposafiri kwenda Cleveland, Ohio, Jumanne, Oktoba 29, kushiriki mdahalo pamoja na mshindani wake Joe Biden. Alisafiri naye pia Jumatano wakati alifanya ziara kwenda Minnesota kwa mkutano wa kampeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.