Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SIASA

Matamshi ya Donald Trump kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais yazua gumzo Marekani

Viongozi wakuu wa chama cha Republican na Democratic nchini Marekani wamelaani matamshi ya rais Donald Trump kuwa huenda asikubali matokeo ya Uchaguzi wa urais utakaofanyika tarehe 3 Novemba.

Kiongozi wa chama cha Republican katika bunge la Senate Mitch McConnell amesema Marekani kuwa mshindi wa Uchaguzi huo ndiye atakayekabidhiwa madaraka kama ambavyo imekuwa baada ya miaka minne.
Kiongozi wa chama cha Republican katika bunge la Senate Mitch McConnell amesema Marekani kuwa mshindi wa Uchaguzi huo ndiye atakayekabidhiwa madaraka kama ambavyo imekuwa baada ya miaka minne. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa chama cha Republican katika bunge la Senate Mitch McConnell kupitia ukurasa wake wa Twitter, amesema Marekani kuwa mshindi wa Uchaguzi huo ndiye atakayekabidhiwa madaraka kama ambavyo imekuwa baada ya miaka minne.

Nancy Pelosi, Spika wa bunge la wawakilishi, ambaye pia ni kiongozi cha chama cha Democratic, amekosoa vikali kauli hiyo ya rais Donald Trump.

Rais Trump, atapambana na Joe Biden wa chama cha Democratic, na mara kadhaa amekuwa akinukuliwa akisema haamini iwapo uchaguzi huo utakuwa huru na haki kutokana na hatua ya wapiga kura wengi kupiga kura kwa njia ya Posta kutokana na janga la Corona.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari wiki hii, alipoulizwa iwapo atakubali kushindwa na kukabidhi madaraka, rais Trump alisikika akisema wataangalia kile kitakachojitokeza.

“Mara kadhaa nimekuwa nikilalamikia mchakato wa upigaji kura na kwamba hali hiyo ni janga.

Kwa takribani mwezi sasa kiongozi huyo ambae anawania muhula wa pili madarakani, amekuwa katika kampeni dhidi ya upigaji kura kwa njia ya barua katika uchaguzi wa Marekani kwa kutumia ukurasa wake wa Twitter na kukosoa wazi kuhusu utaratibu huo.

Mwaka 2016, rais Donald Trump alikataa kujitolea kukubali matokeo ya uchaguzi katika kinyang'anyiro kati yake na mgombea wa Democratic , Hillary Clinton, hatua ambayo alitaja kama shambulio dhidi ya demokrasia ya Marekani.

Hata hivyo alitangazwa kuwa mshindi, licha ya kuwa hakupata kura za wengi ambazo pia bado anatilia shaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.