Pata taarifa kuu
MAREKANI-MAUAJI-HAKI

Mauaji ya Breonna Taylor: Taharuki yatanda Marekani, maafisa 2 wa polisi wajeruhiwa kwa risasi

Maafisa wawili wa Polisi wamepigwa risasi wakati maelfu ya watu wakiandamana katika mji wa Louisville baada ya Mahakama kuamua waliomuua mwanamke mweusi Breonna Taylor hawatachukuliwa hatua.

Makabiliano kati ya waandamanaji na polisi huko Louisville baada ya uamuzi wa mahakama ya Marekani katika kesi ya Breonna Taylor. Septemba 24, 2020.
Makabiliano kati ya waandamanaji na polisi huko Louisville baada ya uamuzi wa mahakama ya Marekani katika kesi ya Breonna Taylor. Septemba 24, 2020. REUTERS/Bryan Woolston
Matangazo ya kibiashara

Hasira za waandamanaji zimesababihwa na Bi Taylor mwenye umri wa miaka 26, kupigwa risasi mara kadhaa baada ya maafisa wa usalama kumvamia nyumbani kwake mwezi Machi.

Kilichochea maandamano hayo ni afisa anayeshukiwa kutekeleza mauji hayo Brett Hankison, amefunguliwa mashataka tofauti, kinyume na matarajio ya wengi , huku maafisa wengine wawili wakisalia huru bila kufunguliwa mashtaka yoyote.

Licha ya kupigwa risasi wakati wa maandamano hayo, ripoti zinasema kuwa hali za maafisa wawili wa polisi sio mbaya sana na wanaendelea kupokea matibabU, huku mshukiwa akimatwa.

Kutoana na vurugu zinazoshuhudiwa, hali ya hatari imetangazwa katika mji wa Louisville na jeshi la akiba kutumwa katika mji huo.

Marekani imeendelea kukumbwa na visa vya mauaji ya watu weusi, vitendo vinavyohusishwa maafisa polisi wazungu, na kuacha maswali mengi kuhusu uwezo wa taifa hilo kupambana na ubaguzi wa rangi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.