Pata taarifa kuu
MAREKANI-BIDEN-KAMALA-SIASA

Kamala Harris akosoa utawala wa Trump

Kamala Harris amekubali uteuzi wa chama chake cha Democratic kuwa mgombea mwenza wa Joe Biden wakati wa Uchaguzi wa urais utakaofanyika mwezi Novemba.

Joe Biden kwenye mkutano wa chama cha Democratic Agosti 19, 2020 huko Wilmington, Delaware.
Joe Biden kwenye mkutano wa chama cha Democratic Agosti 19, 2020 huko Wilmington, Delaware. AP Photo/Carolyn Kaster
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake ya kwanza kwa wajumbe wa chama hicho, katika mkutano mkuu unaofanyika kwa njia ya video, Kamala amekosoa uongozi wa rais Trump na kusema yeye na Biden wataleta uongozi mpya.

Mapema rais wa zamani Barack Obama naye aliwanadi Biden na Kamala, na kumkosa rais Trump kama kiongozi aliyewaangusha Wamarekani na kuwataka wapiga kuwa kumwamini Biden.

Joe Biden anatarajia leo kutoa hotuba rasmi ya kukubali kuwa mgombea wa chama cha Democratic kwenye uchaguzi unaokuja. Katika uchaguzi huo, Biden atakuwa pamoja na Harris Kamala kama mgombea mwenza, anayekuwa mwanamke wa kwanza kutoka jamii ya watu weusi nchini Marekani kuwania wadhifa wa makamu wa rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.