Pata taarifa kuu
MAREKANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya vifo 170,000 vyatbitishwa Marekani

Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Marekani, sasa imevuka 170,000 vinavyohusiana na Covid-19 tangu kuzuka kwa ugonjwa huo nchini humo, kulingana na ripoti iliyotolewa na shirika la habari la Reuters.

Marekani ambayo ina idadi ya visa milioni 5.4 vya maambukizi vilivyothibitishwa, ndio nchi duniani ambayo imeathiriwa zaidi na janga hili.
Marekani ambayo ina idadi ya visa milioni 5.4 vya maambukizi vilivyothibitishwa, ndio nchi duniani ambayo imeathiriwa zaidi na janga hili. REUTERS/Stefan Jeremiah
Matangazo ya kibiashara

Marekani ambayo ina idadi ya visa milioni 5.4 vya maambukizi vilivyothibitishwa, ndio nchi duniani ambayo imeathiriwa zaidi na janga hili.

Nchi hiyo ilirekodi vifo vipya 483 jana Jumapili, Florida, Texas na Louisiana ni majimbo ambayo yameathiriwa zaidi katika nchini Marekani.

Hayo yanajiri wakati dunia sasa ina maambukizi Milioni 21.6M baada ya wagonjwa wapya laki 2 na elfu 68 kuthibitishwa, huku vifo laki 7 na elfu 74 vikithibitishwa baada ya vifo vipya 5,993 kuripotiwa. Hata hivyo wagonjwa Milioni 13.6 wamepona ugonjwa huo hatari.

Hivi karibuni shirika la Afya Dunia, WHO lilizitaka nchi zote kutilia mkazo hatua za kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona.

Shirika hilo lilionya kuwa licha ya jitihada zinazofanyika kutafuta chanjo na dawa ya kupambana na janga la virusi vya Corona, huenda kusiwe na suluhu ya muda mrefu ya kukabiliana na janga hili.

WHO imeendelea kukosoa hatua zilizochukuliwa hivi karibuni na baadhi ya nchi duniani kwa kulegeza masharti ya kukabiliana na janga la Covid-19, ikisema kuwa Covid-19 bado ni tishio duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.