Pata taarifa kuu
MAREKANI-MAUAJI-HAKI

Kifo cha George Floyd chabadilishwa tena kama mauaji, maafisa wanne wa zamani washtakiwa

Mwendesha mashtaka anayechunguza kifo cha George Floyd huko Minneapolis amesema Mmarekani huyo mweusi aliuawa kwa maksudi mwishoni mwa mwezi uliyopita.

Mwendesha mashtaka Keith Ellison, anayesimamia kesi ya kifo cha George Floyd, l, Minnesota, Juni 3, 2020.
Mwendesha mashtaka Keith Ellison, anayesimamia kesi ya kifo cha George Floyd, l, Minnesota, Juni 3, 2020. REUTERS/Eric Miller
Matangazo ya kibiashara

Afisa wa polisi, mwenye umri wa miaka 46, aliyesababisha kifo chake kwa kumbana shingoni kwa goti lake ameshtakiwa kwa "mauaji yasiyokuwa ya kawaida" na maafisa wengine watatu waliokuwepo wakati wa George Floyd alipokamatwa, wameshtakiwa kwa kula njama kwa tukio hilo.

Awali Derek Chauvin, afisa wa zamani wa polisi alishtumiwa kwa mauaji bila kuksudia, na kwa sasa anakabiliwa na kifungo hadi miaka 40 dhidi ya kifungo cha miaka 25 kwa kosa la hapo awali.

Kwa kuongezea mashtaka yake, mwendesha mashtaka Keith Ellison, anayewakilisha mamlaka ya serikali ya Minnesota, ameongeza dhamana ya afisa huyo wa zamani hadi dola milioni moja.

Wakati huo huo aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis amemshutumu Rais Donald Trump, kwa kuleta mgawanyiko na kutumia vibaya mamlaka yake.

Bw. Mattis amesema alighadhibishwa na kufadhaishwa sana na jinsi Bwana Trump alivyoshughulikia maandamano ya hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.