Pata taarifa kuu
MAREKANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Watafiti waonya kutokea zaidi ya vifo 147,000 Marekani

Zaidi ya watu 147,000 wanaweza kufariki dunia kwa ugonjwa wa Covid-19 nchini Marekani hadi mwezi Agosti mwaka huu, wakati hatua za kudhibiti ugonjwa huo zimeanza kuondolewa, watafiti katika Chuo Kikuu cha Washington wameonya.

idadi ya maambukizi imepunguka katika jimbo la New Jersey na Jimbo la New York, ambayo ni  karibu na nusu ya idadi ya vifo.
idadi ya maambukizi imepunguka katika jimbo la New Jersey na Jimbo la New York, ambayo ni karibu na nusu ya idadi ya vifo. REUTERS/Brendan McDermid
Matangazo ya kibiashara

Hii ni idadi iliyoongezwa, baada ya kuripotiwa vifo vipya 10,000, ikilinganishwa na makadirio yaliyotangazwa wiki iliyopita na Taasisi ya Upimaji wa Afya na Tathmini (IHME) ya Chuo Kikuu cha Washington.

Ripoti hii inakuja kuunga mkono wito wa tahadhari wa wataalam wa afya.

Dk Anthony Fauci, mmoja wa washauri wakuu katika Ikulu ya White House, ameliambia bunge kuwa, kuna hatari kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona kurejea tena kwa nguvu iwapo majimbo mbalimnbali nchini humo yataanza kurejesha hali ya kawaida hivi karibuni.

Hayo yanajiri wakati janga la virusi vya Corona sasa limesababisha zaidi ya vifo 290,000 kote duniani kulingana na idadi ya shirika la habari la AFP. Kati ya mabara yote, Ulaya ndiyo iliyoathirika mno ikiwa na zaidi ya vifo 159,000

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.