Pata taarifa kuu
MAREKANI-CORONA-AFYA-UHAMIAJI

Covid-19: Wahamiaji wapigwa marufuku kuingia katika ardhi ya Marekani kwa siku 60

Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini kwenye sheria ya kirais inayositisha visa kwa wahamiaji kuingia nchini humo kwa siku sitini. Hayo yanajri wakati mipaka ya Marekani imefungwa kufuatia kuzuka kwa ugonjwa hatari wa Covid-19 nchini humo.

Donald Trump wakati wa mkutano wa kila siku na waandishi wa habari kuhusu janga la Corona, katika Ikulu ya White, Aprili 20, 2020.
Donald Trump wakati wa mkutano wa kila siku na waandishi wa habari kuhusu janga la Corona, katika Ikulu ya White, Aprili 20, 2020. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

"Rais amesitisha visa kwa wahamiaji ili wafanyakazi, raia wa Marekani wawewa kwanza kunufaika na uchumi kufunguliwa tena," imesema Ikulu ya White House katika taarifa.

Marekani ni nchi ambayo imeathirika zaidi duniani na ugonjwa wa Covid-19, ambao umesababisha vifo vya watu zaidi ya 45,000. Na hatua za kubaki nyumbani, zimewaathiri kiuchumi Wamarekani milioni 22 baada ya kukosa ajira katika wiki za hivi karibuni.

Sheria hii ya rais Trump inahusu visa za kudumu na hiwagusi wa wafanyakazi katika sekta ya afya, kwa wafanyakazi wanaonekana kuwa ni muhimu.

Sheria hiyo haiwagusi pia watu ambao tayari wako nchini Marekani na wanatafuta kibali cha kuruhusiwa kupata ajira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.