Pata taarifa kuu
MAREKANI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Marekani yatangaza vifo vipya zaidi ya 850

Watu 865 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa Covid-9 (Corona) kwa siku moja nchini Marekani. Chuo Kikuu cha Johns Hopkins kimebaini kwamba mpaka sasa ugonjwa hatari wa Covid-19 umeua watu zaidi ya 4,000 nchini Marekani, huku 40% ya vifo hivyo vikiripotiwa katika jimbo la New York.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Donald Trump amewataka raia wa Marekani kuheshimu maagizo yanayowataka kuepuka mikusanyiko ya watu zaidi ya 10, safari zisizo na ulazima, kufungwa kwa mikahawa na baa, na kufanya kazi ukiwa nyumbani.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Donald Trump amewataka raia wa Marekani kuheshimu maagizo yanayowataka kuepuka mikusanyiko ya watu zaidi ya 10, safari zisizo na ulazima, kufungwa kwa mikahawa na baa, na kufanya kazi ukiwa nyumbani. Brendan Smialowski / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo rais wa Marekani Donald Trump ameonya kuwa hali itakuwa mbaya zaidi ndani ya kipindi cha wiki mbili katika kupambana dhidi ya ugonjwa huo hatari, ambao umesababisha vifo vya watu zaidi ya 850 ndani ya masaa 24 nchini Marekani na ambapo mamlaka ya afya ina hofu kwamba idadi ya vifo itazidi 100,000 katika miezi michache ijayo.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Donald Trump amewataka raia wa Marekani kuheshimu maagizo yanayowataka kuepuka mikusanyiko ya watu zaidi ya 10, safari zisizo na ulazima, kufungwa kwa mikahawa na baa, na kufanya kazi ukiwa nyumbani.

"Ni muhimu kabisa raia wa Marekani kufuata mwongozo kwa siku 30 zijazo. Ni suala la maisha au kifo," amesema rais wa Marekani, ambaye alikosolewa kwa kupuuzia kitisho cha ugonjwa wa Corona wakati ulizuka nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.