Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA-USALAMA

Bunge la Venezuela laongozwa na maspika wawili

Mpinzani wa rais wa Venezuela, Nicolas Maduro, Juan Guaido, amechaguliwa tena Spika wa Bunge na wabunge wa upinzani saa chache baada ya mbunge mwingine wa upinzani, Luis Parra, kujitangaza kuwa spika wa bunge.

Juan Guaido amechaguliwa tena Spika wa Bunge la Venezuela na Wabunge wa upinzaji Januari 5, 2020.
Juan Guaido amechaguliwa tena Spika wa Bunge la Venezuela na Wabunge wa upinzaji Januari 5, 2020. REUTERS/Fausto Torrealba
Matangazo ya kibiashara

Juan Guaido amechaguliwa tena kuwa Spika wa Bunge la venezuela katika majengo ya gazeti la El Nacional.

"Ninaapa kwa Mungu na wananchi wa Venezuela kutumikia nchi kwa kuheshimu" Katiba kama "Spika wa Bunge na kaimu rais," amesema Juan Guaido baada ya wabunge 100 kumchaguwa katika uchaguzi ambao wameshiriki wabunge kadhaa wanaosakwa na mahakama kwa kile upinzani unachodai kuwa ni "mpango wa kisiasa".

Luis Parra, amejitangaza kuwa spika wa bunge, katika kikao ambacho Juan Guaido na wabunge wengi wa upinzani haukuweza kuhudhuria, baada ya kuzuiliwa nje ya jengo hilo kwa muda mrefu na polisi.

Mbunge Luis Parra katika Bunge la Venezuela, Januari 5, 2020.
Mbunge Luis Parra katika Bunge la Venezuela, Januari 5, 2020. REUTERS/Manaure Quintero

Upinzani unaomuunga mkono Juan Guaido, ambaye nchi zaidi ya hamsini zinamtambua kama rais wa mpito wa Venezuela, umesema kwa taarifa kwamba mbunge Luis Parra amefanya ishara ya kula kiapo "bila ya kuchaguliwa na idadi ya wabunge ilikuwa haikamiki" na amefanya "mapinduzi ya bunge".

"Huu ni mtego mpya wa kisiasa wa serikali inayoungwa mkono na wahalifu, kwa sababu ndivyo walivyo. Mtu ambaye haheshimu viwango au Katiba ni mshiriki wa utawa wa kiimla, "amesema Juan Guaido.

Rais Nicolas Maduro amemtambua Luis Parra kama Spika mpya wa Bunge.

Luis Parra alifukuzwa katika chama cha upinzani cha Primero Justicia baada ya tovuti ya habari kumshtumu mwezi Desemba kwamba alipokea rushwa kwa kumuunga mkono mjasiriamali wa Colombia ambaye anasemekana alihusika katika kesi ya ufisadi inayohusishwa na uagizaji wa chakula.

Licha ya kutengwa kwake, Luis Parra anadai kuwa bado ni mpinzani wa Nicolas Maduro.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.