Pata taarifa kuu
MAREKANI-UN-USHIRIKIANO-MVUTANO

Marekani yajitoa kwenye Baraza la Haki za Binadamu

Marekani imetangaza kwamba imejitoa kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu huko Geneva. Tangazo hilo lilitolewa Washington na Waziri wa Mashauriano ya Kigeni Mike Pompeo na Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley.

Nikki Haley, balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, hapa ilikua mwezi Januari 2018, katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa.
Nikki Haley, balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, hapa ilikua mwezi Januari 2018, katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa. REUTERS/Lucas Jackson
Matangazo ya kibiashara

Taasisi hii ya Umoja wa Mataifa iliundwa mwaka 2006 ili kuendeleza haki za binadamu duniani kote. Marekani inaishtumu kutokana na unyonge dhidi ya Israeli.

Wawili hao walitoa maeneo ya kashfa dhidi ya taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa wakiita kuwa ni taasisi ya wajinga, wenye ubinafsi, chanzo cha matatizo katika nchi mbalimbali.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley, alitoa tishio hilo la kujitoa kwa Marekani kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu tangu mwaka mmoja uliopita. "Marekani itajitoa rasmi kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa. Ningependa kusema waziwazi kwamba mpango huu hauashirii kujitoa kwa ahadi zetu kuhusu haki za binadamu, " amesema Nikki Haley.

Nikki Haley mara kwa mara amekua akilaumu taasisi hiyo kuwa na upendeleo fulani, akiishtumu kufanya sera za za ubaguzi kwa baadhi ya nchi: "Baraza la Haki za Binadamu lilipitisha maamuzi matano dhidi ya Israeli. Hiyo ni zaidi ya maazimio yaliyopitishwa dhidi ya Korea ya Kaskazini, Iran na Syria, " ameongeza balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa.

Tangazo hilo linakuja baada ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Kamishna wake Mkuu wa Haki za Binadamu kukosoa namna familia za wahamiaji zinavyonyimwa nchini Marekani. Katika siku za hivi karibuni, utawala wa Trump unakabiliwa na shutma kali kutoka ulimwenguni. Utawala wa Trump unashtumiwa kukiuka haki za binadamu kwa kutenganisha wahamiaji na watoto wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.