Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-KASKAZINI-MAREKANI

Marekani, Korea Kusini zatangaza kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi

Nchi za Korea Kusini na Marekani zimethibitisha kuendelea mbele na mazoezi makubwa ya kijeshi kati ya nchi hizo mbili yaliyopangwa kuanza April Mosi mwaka huu, hatua ambayo huenda ikatatiza mazungumzo kati yas Marekani na Korea Kaskazini.

Ndege za kivita za Marekani zikishusha wanajeshi kwenye kambi ya jeshi ya Osan nchini Korea Kusini tayari kujiandaa kwa mazoezi ya pamoja. March 20, 2018.
Ndege za kivita za Marekani zikishusha wanajeshi kwenye kambi ya jeshi ya Osan nchini Korea Kusini tayari kujiandaa kwa mazoezi ya pamoja. March 20, 2018. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mazoezi haya ya kijeshi ndio yamekuwa chanzo cha sintofahamu ya kwenye eneo la rasi ya Korea, mazoezi ambayo Korea Kaskazini inaona ni kama njama za nchi hizo kutaka kuishambulia.

Mazoezi hayo yalikuwa yaanze mwezi Machi mwaka huu lakini yalilazimika kusogezwa mbele kuepusha mvutano wa kidiplomasia wakati wa michezo ya bardi ya Olimpiki.

Jumla ya wanajeshi laki tatu hushiriki kwenye mazoezi haya ya kijeshi, ikiwa ni mazoezi yanayohusisha wanajeshi wengi zaidi pamoja na zana za kijeshi.

Tangazo la kufanyika kwa mazoezi haya linatolewa wakati huu kukiwa na juhudi zinazoendelea kujaribu kuandaa mkutano kati ya rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un.

Korea Kaskazini tayari imeonesha nia ya kuachana na mpang wake wa Nyuklia, na hii ni kwa mujibu wa maofisa wa Korea Kusini.

Mpaka sasa hakuna taarifa zaidi zilizotolewa na hata Korea Kaskazini haijasema chochote kuhusiana na mazungumzo hayo, ambapo itakuwa ni mara ya kwanza kwa rais wa Marekani aliyeko madarakani kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini.

Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini Ri Yong-ho juma lililopita alikuwa nchini Sweden katika kile kinachoonekana ni mazungumzo ya kuchagua eneo la viongozi hao kukutana.

Ingawa Marekani na Korea Kusini zinasema mazeozi haya hayalengi kuichokosa Korea Kaskazini, wadadisi wengi wa mambo wanaona kuwa kufanyika kwa mazeozi haya kutaibua tena sintofahamu kati ya nchi hizo mbili Jirani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.