Pata taarifa kuu
MAREKANI-SIASA

Mshauri wa karibu wa Trump aachia ngazi

Mmoja wa mashauri wa karibu wa Rais Trump wa muda mrefu na Mkurugenzi wa mawasiliano, Hope Hicks, ameamua kujiuzulu kwenye nafasi yake, ikulu ya White House imesema.

Hope Hicks baada yakusikilizwa kuhusu kesi ya Urusi kuingilia katika uchaguzi wa urais wa Marekani mnamo Februari 27, 2018 Washington.
Hope Hicks baada yakusikilizwa kuhusu kesi ya Urusi kuingilia katika uchaguzi wa urais wa Marekani mnamo Februari 27, 2018 Washington. REUTERS/Leah Millis
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa kampeni za uchaguzi, Hope Hicks alifanya kazi kama khatibu wa mawasiliano. Alichukua nafasi ya kuungoza idara ya mawasiliano ya White House mwezi Agosti mwaka jana, baada ya Anthony Scaramucci kufutwa kazi.

Kwa mujibu wa afisa mmoja ambaye hakutaja jina lake, Hope Hicks amewaambia wafanyakazi wenzake kuwa anaona ametimiza wajibu wake katika ikulu ya White House.

Hope Hicks, mwana mitindo, mwenye umri wa miaka 29, alikua karibu na Donald Trump kwa miaka mingi.

Bi Hicks ni mtu wa nne aliyeshika nyadhifa ya mkurugenzi wa mawasiliano, baada ya Anthony Scaramucci, Sean Spicer na Mike Dubke.

Msemaji wa White House Sarah Sanders amethibitisha taarifa hiyo lakini amesema haijulikani Bi Hicks ataondoka lini.

Hata hivyo Bi Sanders amefutilia mbali madai ya kuwa hatua hio inahusiana na ushahidi ambao Bi Hicks aliutoa kukiri kusema uongo wa wazi kwa niaba ya Bw Trump mbele ya kamati bunge la Congress.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.