Pata taarifa kuu
MAREKANI-MHUBIRI

Mhubiri maarufu Billy Graham afariki dunia akiwa na miaka 99

Mhubiri maarufu  nchini Marekani na duniani Billy Graham amefariki duniani akiwa na umri wa miaka 99.

Billy Graham aliyekuwa Mhubiri maarufu duniani
Billy Graham aliyekuwa Mhubiri maarufu duniani REUTERS/Shannon Stapleton/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Graham alifahamika sana duniani kutokana na Uinjilisti alioufanya na mahubiri aliyotoa katika nchi mbalimbali duniani kuanzia miaka ya 1950.

Alianza huduma ya kuhubiri baada ya kutawazwa akiwa na miaka 21, mwaka 1939.

Familia yake imesema alifariki dunia akiwa nyumbani kwake katika jimbo la Carolina Kaskazini.

Graham anaelezwa kuhubiri kwa zaidi ya miaka 60, na kubadilisha mitizamo ya Mamia ya Mamilioni ya watu waliokubali ujumbe wake.

Mbali na mahubiri akiwa katika viwanja mbalimbali vya michezo na ukumbi, alitumia pia runinga na redio kuhubiri.

Amesufiwa kama Mhubiri mwenye ushawishi mkubwa katika karne ya 20.

Wakati wote wa uhai wake, alikuwa na urafiki wa karibu na marais wote wa Marekani kutoka kwa rais Truman, Nixon hadi Barrack Obama.

Rais Donald Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema, Graham alikuwa mtu wa kipekee na Wakiristo na watu wa dini nyingine, watamkosa sana.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.