Pata taarifa kuu
CANADA-UGAIDI

Canada kukabiliana na msimamo mkali wa wanajihadi

Canada inapania kukabiliana na msimamo mkali wa vijana kwa itikadi ya wanajihadi, baada ya kifo cha mmoja wao ambaye aliapa kushirikiana na kundi la Islamic Statepamoja na mashambulizi mawili dhidi ya wanajeshi mwaka 2014, serikali imetangaza Jumatatu.

Askari wa Syria wakichoma moto bendera ya kundi la Islamic State baada ya vikosi vya Syria kudhibiti siku moja kabla mji wa al-Qaryatain katika jimbo la Homs, Syria, Aprili 4, 2016.
Askari wa Syria wakichoma moto bendera ya kundi la Islamic State baada ya vikosi vya Syria kudhibiti siku moja kabla mji wa al-Qaryatain katika jimbo la Homs, Syria, Aprili 4, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Kituo "kwa ajili ya cha uhamasishwaji na mapambano dhidi ya msimamo mkali" kitaundwa nchini Canada, " amesema Ralph Goodale, Waziri wa Usalama wa Raia.

ufuatia "shambulizi la kigaidi lililohindwa wiki iliyopita" katika mji wa Strathroy, mji mdogo kusini mwa jimbo la Ontario (katikati), serikali ya Canada ina "wasiwasi kuhusu vijana wanaovutia na itikadi za ukaidi na zenye msimamo mkali ambazo zinakuza ghasia. "

Jumatano jumaililopita katika mji wa Strathroy, raia wa Canada , mwenye umri wa miaka 24 aliuawa baada ya kulipua kilipuzi nyuma ya teksi iliyokua ilizungukwa na vikosi vya usalama.

Zaidi ya raia mia mmoja kutoka Canada wameungana na IS

Tayari katika mwaka 2014, watu wawili wenye msimamo mkaliwaliendesja shambulizi katika mji wa Quebec na katika mji mkuu wa Ottawa ambapo askari wawili waliuawa.

Zaidi ya watu mia mmoja kutoka Canada wamemejiunga na wapiganaji wa kundi la IS nchini Syria na Iraq katika miaka ya hivi karibuni na wengi walizuiliwa katika mipaka kabla ya kuelekea Uturuki.

Waziri Ralph Goodale alikuwa Jumatatu katika mji wa Montreal kuzuru kituo cha kuzuia msimamo mkali ambacho uongozi wa mji huo umeanzisha baada ya vijana saba kuelekea Uturuki mwezi Januari 2015, na kukamatwa katika uwanja wa ndege wengine 10 walio na umri kati ya 15 hadi 18 wiki kadhaa baadaye. Kituo kama hiki pia kinapatikana katika mji wa Calgary, katika jimbo la Alberta, magharibi mwa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.