Pata taarifa kuu
URUSI-MAREKANI-SYRIA-USHIRIKIANO-USALAMA

Vita Syria: Putin ampokea Kerry

Rais wa Urusi Vladimir Putin amempokea katika Ikulu ya Kremlin Jumanne hii waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ili asikie"mapendekezo" ya Marekani yanayolenga kuendelea katika utatuzi wa mgogoro wa Syria kabla ya mkutano wa kimataifa Ijumaa wiki hii mjini New York.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na Rais wa Urusi Vladimir Putin katika Ikulu ya Kremlin mjini Moscow, Desemba 15, 2015.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na Rais wa Urusi Vladimir Putin katika Ikulu ya Kremlin mjini Moscow, Desemba 15, 2015. AFP/POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkutano kati ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani na Rais wa Urusi yameanza saa 9:30 alaasiri saa za kimataifa, huu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov akishiriki mkutano huo.

"Unajua kwamba tunatafuta ufumbuzi wa migogoro iliyokithiri", Putin amesema akimaanisha vita nchini Syria, ambavyo tangu mwaka 2011 vimegharimu maisha ya zaidi ya watu 250,000, na kusababisha mamilioni ya raia wa Syria kuyahama makazi yao, huku kukiibuka kundi la Islamic State.

Kerry kwa upande wake, amekaribisha "juhudi nzuri ya ushirikiano" kati ya Moscow na Washington, akisema kuwa "anapongeza mambo yote yanayofanywa na (nchi hizo mbili) hadi sasa."

Washington ina matumaini na Kremlin kwa kumleta mshirika wake wa jadi, Rais Bashar al-Assad katika meza ya mazungumzo pamoja na upinzani wa Syria ili kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mkutano kati ya Kerry na Putin ulitanguliwa na saa tatu ya mazungumzo kati ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani na mwenzake wa Urusi.

"Lavrov amenitaarifu kwa undani mapendekezo yenu pamoja na baadhi ya matatizo ikiwa ni pamoja na mazungumzo, vinahitajika", Putin amesema.

Muda mfupi kabla ya mazungumzo na mwenzake, waziri wa mambo ya nje wa Marekani amesema ana matumaini ya "maendeleo" na "maelewano" katika suala la Syria huku mwenzake wa Urusi akitaka mazungumzo yenye "kujenga".

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.