Pata taarifa kuu
MAREKANI-NASA-SAYARI

NASA: "ushahidi wa maji maji juu ya sayari ya Mars"

Shirika la Marekani la Utafiti wa Anga (NASA) limesema Jumatatu wiki hii kuwa na ushahidi unaoonyesha uwepo wa maji maji kwenye sehemu ya nje ya sayari ya Mars. Ugunduzi ambao umeleta mapinduzi ya uelewa wa sayari nyekundu.

Picha iliyotolewa na NASA Septemba 27, 2015, inaonyesha sehemu ya nje ya sayari ya Mars.
Picha iliyotolewa na NASA Septemba 27, 2015, inaonyesha sehemu ya nje ya sayari ya Mars. AFP/NASA/AFP
Matangazo ya kibiashara

" Mars si sayari kavu, yenye ukame inavyoonekana kuwa hadi sasa ", amesema Jim Green, mmoja wa wakurugenzi wa NASA, katika mkutano na waandishi wa habari.

" Haya ni maendeleo muhimu ambayo yanaonyesha kuthibitisha kwamba maji yanayofanana kama yale ya mito yanatiririka kwenye sehemu ya nje ya sayari ya Mars " pia amesema John Grunsfeld, msimamizi msaidizi wa NASA.

Maendeleo ya hivi karibuni, yaliyopatikana kutokana na picha zilizotolewa na uchunguzi wa chombo cha NASA orbiter kwa kutumia kifaa cha spectrometer "kimesaidia sana" kwa ugunduzi wa uwepo wa maji maji juu ya sayari ya Mars na kwa siku hizi, wanasayansi kutoka Ufaransa na Marekani wamehitimisha kazi yao.

Katika siku za nyuma sayari ya Mars ilikuwa sawa na dunia pamoja na maziwa, mito viliyochimba mabonde na bahari kubwa, amekumbusha Jim Green, mkuu wa kitengo cha sayansi za dunia katika NASA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.