Pata taarifa kuu
MAREKANI-PAPA-USHIRIKANO

Papa Francis ziarani Marekani

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Ppa Francis ameanza ziara yake nchini Marekani. Papa Francis alipokelewa na rais Barrack Obama na katika ziara yake nchini humo atakuwa jijini Washington DC, New York na Philadelphia.

Papa Francis alikaribishwa mjini Washington Jumanne Septemba 22 na Rais wa Marekani Barack Obama na familia yake katika kambi ya jeshi ya AndrewsAir Force Base.
Papa Francis alikaribishwa mjini Washington Jumanne Septemba 22 na Rais wa Marekani Barack Obama na familia yake katika kambi ya jeshi ya AndrewsAir Force Base. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Akiwa Marekani, kiongozi huyo wa Kanisa katoliki atakutana na wamini wa Kanisa hilo, atahotubia pia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kuzungumzia maswala yanayoikumba dunia ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa na machafuko yanayoendelea katika nchi mbalimbali.

Ni kwa mara ya kwanza kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki kufanya ziara nchini Marekani.

Papa alitamatisha ziara yake ya masaa 72 Jumanne wiki hii nchini Cuba (kisiwa cha kikomunisti), nchi ambayo ilifufua hivi karibuni uhusiano wake na Marekani kwa mchango mkubwa wa msuluhishi kutoka Vatican na Papa kutoka Argentina.

Papa Francis alipokelewa na kusherehekewa kwa muda wa siku nne katika mji wa Santiago nchini Cuba, ambapo kunapatikana bandari kubwa ya kisiwa hicho, kulikoanzishwa harakati za ukombozi wa Cuba, karibu na kambi ya majeshi ya Marekani ya Guantanamo.

Papa mwenye umri wa miaka 78 sasa, alisherehekea Misa ya mwisho ya ziara yake katika mahali patakatifu pa Bikira "del Cobre", katika milima ya kijani karibu na mji, na ambapo siku moja kabla aliongoza maombi kwa mustakabali wa watu wa Cuba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.