Pata taarifa kuu
MAREKANI-CHARLESTON-MAUAJI-USALAMA

Marekani: mshukiwa wa mauaji ya Charleston akamatwa

Dylann Roof, mshukiwa wa mauaji ya watu tisa katika Kanisa lenye waumini wengi kutoka jamii ya watu weusi jijini Charleston, nchini Marekani, amekamatwa, mkuu wa polisi jijini humo amethibitisha.

Picha ya mshukiwa muuaji, Dylann Roof iliyopakuliwa kutoka kwaakaunti yake ya Facebook.
Picha ya mshukiwa muuaji, Dylann Roof iliyopakuliwa kutoka kwaakaunti yake ya Facebook. Facebook
Matangazo ya kibiashara

Dylann Roof, mwenye umri wa mika 21, amekamatwa katika mji wa Shelby katika jimbo la North Carolina, kwenye umbali wa kilomita 400 na eneo la tukio, wakati wa ukaguzi wa magari, kwa mujibu wa mkuu polisi, Gregory Mullen. Vikosi vya usalama jijini Charleston vitajielekeza katika mji wa Shelby kwa minajili ya kumhoji mshukiwa, ameongeza mkuu wa polisi.

Kijana huyo mzungu, inasemekana kuwa alikua katika kKanisa hilo Jumatano jioni kwa muda wa saa moja, na inasadikiwa kuwa huenda alikua pamoja na viongozi wa Kanisa. Mwanamke mmoja ambaye alishuhudia tukio bilo, amesema kuwa kwamba alimuona Dylann Roof, akisimama na kuanza kufyatua risasi. Mwanamke huyo amebaini kwamba baada ya mauaji hayo kijana huyo alimueleza kuwa hatomfanya chochote ili aweze kuhadithia kilichotokea, gazeti la kila wiki la Post and Courier la nchini Marekani limeeleza. Mchungaji Clementa Pinckney, seneta wa zamani wa jimbo la South Carolina na mchungaji wa Kanisa la Emanuel African Methodist Episcopal Churc tangu mwaka 2010 pamoja na dada yake ni miongoni mwa watu waliouawa.

Kabla ya kijana huyo kukamatwa, mkuu wa polisi aliyataja mauaji hayo kuwa ni uhalifu wa kibaguzi, uliyochochewa na chuki.

" Tuna watu tisa waliouawa tisa kwa uhalifu wa kikabila uliyochochewa na chuki. . Tunamtafuta kijana mzungu mwenye umri wa miaka 21, ana nywele nyeupe laini, ambaye ni hatari. Tumemeweka uwezo wa kutoshaili kuhakikisha kuwa tumempata mtu huyo aliyefanya uhalifu wa aina hii ", amesema Gregory Mullen.

Polisi ya Charleston ilikua imesambaza picha za kijana huyo ziliyonaswa na kamera ya ulinzi. Alionekana akiondoka katika eneo la tukio na gari nyeusi.

Katika hotuba fupi iliyopeperushwa hewani kwenye televisheni za Marekani, rais wa Marekani Barack Obama ametoa wito wa kukabiliana dhidi ya silaha, huku akilani mauaji yaliyotokea katika kanisa la Emanuel African Methodist Episcopal Churc.

Janga jipya kwa kwa jamii ya Wamarekani weusi

Hili ni janga jipya kwa jamii ya watu weusi wa jimbo la Souht Carolina. Mwezi Aprili, Walter Scott, kijana mweusi ambaye hakua na silaha aliuawa kwa kupigwa risasi nane mgongoni. Askari polisi mzungu ndiye aliye husika na mauaji hayo. Itafahamika pia kwamba mwaka mmoja uliyopita kijana mwengine mweusi, aliuawa katika mji wa Ferguson.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.