Pata taarifa kuu
MAREKANI-MAGEUZI-SHERIA-USALAMA

Marekani: mageuzi ya Sheria ya Uzalendo yapitishwa na Seneti

Baraza la Seneti la Marekani hatimaye limepitisha mageuzi ya sheria ya Uzalendo (Patriot Act) iliopendekezwa na utawala wa Obama, sawa na Baraza la Wawakilishi. Wakati huo huo, rais wa Marekani, Barack Obama amesaini sheria hiyo.

Baada ya miezi kadhaa ya mjadala, Baraza la Seneti hatimaye limepitisha mageuzi ya sheria ya Uzalendo (Patriot Act), inayoitwa sheria ya Uhuru (Freedom Act).
Baada ya miezi kadhaa ya mjadala, Baraza la Seneti hatimaye limepitisha mageuzi ya sheria ya Uzalendo (Patriot Act), inayoitwa sheria ya Uhuru (Freedom Act). REUTERS/Gleb Garanich
Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa makampuni ya simu yatakua na jukumu la kuhifadhi data za mawasiliano. Mageuzi ambayo Ikulu ya Marekani imeyataja kuwa ni makubwa. Mjadala kuhusu usalama wa ndani uliyodumu miezi kadhaa sasa umemalizika.

Kusimamishwa kwa Sheria ya Uzalendo kulidumu chini ya masaa 48. Idara za Upelelezi za Marekani zitaanza kazi yao ya ukusanyaji wa takwimu, ambapo makampuni ya simu yatahusika na kuhifadhi data za mawasiliano.

Mipaka imewekwa katika sheria hiyo mpya, iitwayo Sheria ya Uhuru, ili kuzuia jaribio lolote la kuingilia maisha ya wananchi ambao hawatuhumiwi chochote. Maseneta wa kihafidhina wamedhihirisha tofauti zao. Kati ya vyama vya mrengo wa kulia ambavyo vilitaka nakala ya sheria hiyo ihifadhiwe kwa muda uliyopangwa siku moja baada ya Septemba 11, na mrengo wa katikati kulia (libertarian), ambao walitaka kuachana moja kwa moja na mfumo wowote wa kurekodi mawasiliano ya simu. Hakuna maelewano yaliyoafikiwa kati ya pande hizo mbili.

Sheria iliyopendekezwa na utawala wa Barack Obama hatimaye imepitishwa kulingana na idadi ya Wabunge na Maseneta wanaohitajika. Baada ya sheria hiyo kupitishwa na Baraza la Wawakilishi na Seneti, Barack Obama amesaini sheria hiyo na kuwa sheria rasmi. Mageuzi ambayo yametajwa na Ikulu ya Marekani kuwa ni " makubwa ", baada ya kuvuja kwa siri za Marekani ziliyotolewa na Edward Snowden, miaka miwili iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.