Pata taarifa kuu
UFARANSA-CUBA-HAITI-DIPLOMASIA

François Hollande awasili Haiti

Baada ya ziara ya siku moja nchini Cuba, rais wa Ufaransa François Hollande, amewasili leo Jumanne nchini Haiti, hatua ya mwisho ya ziara yake katika ukanda wa Amerika ya Kusini.

Rais wa Ufaransa François Hollande (kushoto), rais wa Haiti Michel Martelly (katikati), waziri mkuu wa Haiti  Evans Paul na balozi wa Ufaransa Haiti Elisabeth Beton-Delegue,Port-au-Prince, Mei 12 mwaka 2015.
Rais wa Ufaransa François Hollande (kushoto), rais wa Haiti Michel Martelly (katikati), waziri mkuu wa Haiti Evans Paul na balozi wa Ufaransa Haiti Elisabeth Beton-Delegue,Port-au-Prince, Mei 12 mwaka 2015. REUTERS/Andres Martinez Casares
Matangazo ya kibiashara

Katika ziara hiyo nchini Haiti, rais Hollande atakutana kwa mazungumzo na rais wa nchi hiyo Michel Martelly.

François Hollande ameahidi kuimarisha msaada wake kwa ajili ya ujenzi baada ya tetemeko kali la ardhi la mwaka 2010 na kuunga mkono mfumo wa kisasa wa shule nchini Haiti.

Rais Hollande anafanya ziara katika baadhi ya mataifa ya Amerika ya Kusini katika hali ya kufufua na kukuza mahusiano kati ya nchi hizo na Ufaransa.

Jumapili jioni juma hili lililopita, François Hollande alifanya ziara ya kikazi nchini Cuba, ikiwa ni ziara ya kwanza ya rais wa Ufaransa tangu nchi ya Cuba kupata uhuru wake mwaka 1898.

François Hollande akiwasili Havana, Cuba, Mei 10 mwaka 2015.
François Hollande akiwasili Havana, Cuba, Mei 10 mwaka 2015. AFP PHOTO / ADALBERTO ROQUE

Awali Rais wa Ufaransa alieleza kuwa ziara yake nchini Cuba ni ya kihistoria. François Hollande ni rais wa kwanza kutoka nchi za Magharibi kuwasili nchini Cuba tangu kudorora kwa mahusiano kati ya Marekani na Cuba.

Itafahamika kwamba hivi karibuni Marekani na Cuba vilifufua uhusiano wa kidiplomasia, baada ya kudororo kwa kipindi cha zaidi ya miaka hamsini iliyiopita. Ufaransa ilipiga kura mara kadhaa kwa kuunga mkono Umoja wa Mataifa, ili Marekani iondoleye vikwazo Cuba. “ Tunapaswa kutumia fursa ya yale yaliyopita kwa kuwa wa kwanza kuanzisha mahusiano katika masuala ya uchumi na Cuba ”, François Hollande alilielezea jarida la Jumapili ( Journal du dimanche).

Mbali na mahusiano ya kidiplomasia na nia ya kudumisha uhusiano kati ya Ufaransa na Cuba, rais wa Ufaransa anapania kuanzisha uhusiano na Cuba katika masuala ya biashara. Makampuni ya Ufaransa huenda yakafanikiwa katika mahusiano hayo kati ya nchi hizi mbili. Hata hivyo Ufaransa inatazamia pia katika hatua ya pili, kujadiliana na Cuba kuhusu masuala ya haki za binadamu. Cuba imekua ikilaumiwa kuvunja haki za binadamu, na kujihusisha vitendo vya unyanyasaji dhidi ya binadamu.

Baadhi ya viongozi na wamiliki wa makampuni ya Ufaransa wanaandamana na Rais Hollande katika ziara yake anayoifanya katika baadhi ya mataifa ya Amerika ya Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.