Pata taarifa kuu
MAREKANI-MISSOURI-MAUAJI-ANTONIO-USALAMA-HAKI

Kijana wa Kimarekani mwenye asili ya Afrika auawa Missouri

Antonio Martin, kijana mwenye umri wa miaka 18, raia wa Marekani mwenye asili ya kiafrika ameuawa na polisi Jumanne Desemba 23 jioni kwenye kituo cha mafuta katika kata ya Berkeley, katika kitongoji cha St. Louis nchini Marekani.

Maandamano ya raia wa Marekani kutoka jamii ya Kiafrika katika mji wa Ferguson, kufuatia uamuzi wa majaji,wa kutomtia hatiani afisa wa polisi aliye muua kwa kumpiga risasi kijana Michael Brown.
Maandamano ya raia wa Marekani kutoka jamii ya Kiafrika katika mji wa Ferguson, kufuatia uamuzi wa majaji,wa kutomtia hatiani afisa wa polisi aliye muua kwa kumpiga risasi kijana Michael Brown. REUTERS/Jason Redmond
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo limetokea karibu na mji wa Ferguson, ambako kijana mwengine mwenye asili ya kiafrika, Michael Brown, aliuawa mwezi Agosti mwaka 2014, na kupelekea kuzuka kwa machafuko.

Taarifa ya kifo cha Antonio Martin imezua moja kwa moja maandamano na vurugu katika jimbo la Missouri.

Kifo cha kijana huyo kimefika wakati ambapo mvutano umekua ukishuhudiwa kati ya jamii mbalimbali nchini Marekani. Ndani ya masaa machache tu, hashtag #AntonioMartin imekuwa imeshatumiwa zaidi ya mara 210 000 kwenye mtandao.

Kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, ujumbe wa kuunga mkono, hasira pamoja na salamu za rambirambi umekua ukitolewa ns watu kutoka maeneo mbalimbali nchini Marekani na kungineko duniani.

Wakiwa ni wenye masikitiko na hasira, watumiaji wa intaneti duniani wamenyooshea kidole tukio ambalo wanaona kwa mara nyingine kuwa halikuzingatia haki. Mazingira ya kifo cha Antonio Martin bado ni ya kutatanisha .

Wakati ambapo uchunguzi ukiendelea, watumiaji wa intaneti wameanzisha uchunguzi na kujaribu kutofautisha ukweli na uongo. Kwani kwenye Intaneti, taarifa mbili zinakinzana kuhusu tukio hilo : ile iliyotolewa na polisi katika kata ya St. Louis pamoja na ile, kwa mujibu wa mashahidi, Antonio Martin hakuwa na silaha.

Kwenye akaunti zake za Facebook na Twitter, polisi ya kata ya St. Louis, ambayo imeanzisha uchunguzi, ilitoa taarifa kuwa Antonio Martin "huenda alimnyooshea bunduki afisa wa polisi ambaye hakusita kumfyatulia risasi, baada ya kuona kuwa maisha yake yako hatarini.

Kulingana na taarifa nyingine, mtu mwingine aliyekuwa ameandamana na Antonio Martin katika kituo cha mafuta alikimbia baada ya kusikia mlio wa risasi.

Uchunguzi umeanzishwa. Tukio hili jipya la kifo cha kijana huyo limepelekea wakaazi wa jimbo la Missouri kuwa ni wenye hasira. Kundi moja la waandamanaji limekusanyika karibu na eneo la tukio. Wakati huo huo makabiliano yalitokea kati ya waandamanaji na polisi, ambapo gari la polisi limechomwa moto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.