Pata taarifa kuu
MAREKANI-EBOLA-UN-AFRIKA-Afya

Marekani yaendelea kupambana dhidi ya Ebola

Wanajeshi wa Marekani ambao wanarejea kutoka katika maeneo yaliyoathirika na Homa ya Ebola Afrika ya Magharibi, watawekwa karantini.

Muuguzi , Kaci Hickox, ambaye aliomba kuewekwa karantini baada ya kurejea Marekani akitokea Sierra Leone, ameruhusiwa kuondoka hospitalini.
Muuguzi , Kaci Hickox, ambaye aliomba kuewekwa karantini baada ya kurejea Marekani akitokea Sierra Leone, ameruhusiwa kuondoka hospitalini. REUTERS/Steve Hyman/handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hao watafikia katika kambi ya wanajeshi wa Marekani ilioko nchini Italia kabla ya kuingia marekani.

Wakati huo huo, muuguzi aliye kuwa akihudumu nchini Sierra Leone, ambaye aliwekwa karantini kwa hiari yake katika hospitali ya New Jersey, ameruhusiwa kuondoka hospiatli.

Utawala umeshindwa kutekeleza hatua ziliyochukuliwa za kukabiliana na maambukizi ya Ebola kufuatia hofu ya wananchi kuhusu Homa hiyo ya Ebola. Wanajeshi wanaorejea nchini Marekani wakitokea katika mataifa ya Afrika ya Magharibi yanayoendelea kuathirika na Ebola, watakua wakifikia katika kituo cha uchunguzi.

Hata hivo hivo Marekani imetolea wito kwa raia kuwa watulivu na kutowabughuzi wafanyakazi katika sekta ya Afya.

Wakati huo huo Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa yuko nchini Ethiopia kujadili mlipuko wa Ebola.

Akiwa ameandamana na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim Katibu mkuu Ban Ki Moon anakutana na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Jumanne Oktoba 28 asubuhi, kuzungumzia mlipuko huo na hali ya usalama katika mataifa ya pembe ya Afrika.

Ban na Jim pamoja na wawakilishi wa mashirika mengine ya kimataifa, wako kwenye ziara hiyo, kutembelea nchi za Ethiopia, Kenya na Djibouti kuangalia masuala ya maendeleo na amani.

Tayari Umoja wa Mataifa na Benki ya dunia vimetangaza ufadhili wa Dola bilioni nane, kusaidia mataifa hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.