Pata taarifa kuu
UN-MAREKANI-IS

Raia wa kigeni miongoni mwa wapiganaji wa IS

Barack Obama anaongoza kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, siku moja baada ya mashambulizi ya anga ya jeshi la Marekani nchini Syria.

Lutter contre le jihad passe aussi par un combat idéologique sur Internet, selon l'UE.
Lutter contre le jihad passe aussi par un combat idéologique sur Internet, selon l'UE. AFP PHOTO / YOUTUBE
Matangazo ya kibiashara

Kikao hicho kinatathmini hali ya hatari inayojiri wakati huu kufuatia kuwepo kwa wapiganaji wa kigeni katika kundi la Dola la Kiislam, pamoja na makundi mengine ya kigaidi kama Khorassan, kundi ambalo lililengwa katika mashambulizi ya jeshi la Marekani Septemba 22 mwaka 2014.

Imeonekana dhahiri kwamba watu hao wamekua wakisafiri na kujiunga na makundi ya kigaidi hususan IS wakitumia passport za mataifa ya Ulaya na Marekani, jambo ambalo Baraza la Usalama la Umoja wa Kimataifa linaona kwamba ni tishio kwa ulimwengu hasa Marekani.

Idadi ya wapiganaji hao inakadiriwa kufikia 12,000 walioorodheshwa katika makundi ya kijihad.

Marekani inatazamia kuidhinisha sheria inayozuiya watu kusafiri kwa kujiunga na makundi ya kigaidi, lakini tatizo ni kutambua uraia halisi wa watu hao.

zaidi ya raia 100 wa Marekani wamejiunga na wapiganaji wa Dola la Kiislam. Inaaminika kwamba raia wa Marekani kutoka jamii ya wa Somalia wamekua wakilengwa kupelekwa kujiunga na makundi hayo ya kigaidi. Baadhi ya vijana wa jimbo la Minneapolis walijikuta nchini Somali na Syria.

Abdirizik Bihi, ambaye alianzisha hivi karibuni katika jimbo la Minnesota kituo cha jamii kwa jamii ya raia wa Somalia ambao wamekua wakiogopa kubaguliwa. " Kwa kweli tatizo si kubwa, ni kati ya watu 40 na 50”, amesema Abdirzik Bihi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.