Pata taarifa kuu
SYRIA-Usalama

 Syria yafurahia ushindi wake dhidi ya waasi

Utawala wa Syrie una imani na ushindi dhidi ya waasi baada ya kusaidiwa na washirika wao, hususan Urusi, waziri wa mambo ya nje wa Syria amemthibitishiya mwenzake wa Urusi katika barua aliyomuandikia.

Wafuasi wa Bashara al Assad wakisheherekea ushindi wa jeshi dhdi ya waasi.
Wafuasi wa Bashara al Assad wakisheherekea ushindi wa jeshi dhdi ya waasi. © Reuters/Sana
Matangazo ya kibiashara

“Ushindi wa Syria umepatikana kutokana na usaidizi wa raia na washirika wake, hususan Urusi”, waziri Walid Mouallem amesema katika barua aliyomuandikia Seguei Lavrov, kufuatia maadhimisho ya miaka 70 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili.

“Viongozi wa Syria na raia wanatambua vema na kupongeza msimamo wa Urusi kwa kuiunga mkono Syria kwa vita vya kimataifa vilivyoanzishwa dhidi yake kwa kupambana na ugaidi, ameendelea kusema Mouallem katika barua hiyo.

Utawala wa Bashar Al Assad haujatambua kwamba kuna maandamano na mapigano yanayoendeshwa na raia kwa kuung'oa serikali ya Assad, bali inadai kwamba ni ugaidi. Machafuko hayo yamesababisha vifo vya watu 170.000 na wengine zaidi ya milioni 9 wameyahama makaazi yao.

Wapiganaji wa kundi la Liwa al-Islam,linaloshirikiana na jeshi la Syria katika vita dhidi ya waasi.
Wapiganaji wa kundi la Liwa al-Islam,linaloshirikiana na jeshi la Syria katika vita dhidi ya waasi. REUTERS/Molhem Barakat

Mouallem amesema Jeshi la Syria limeamua kuvunja ugaidi kwa kulinda taifa lake na kuimarisha usalama wa eneo lote linaoshikiliwa na waasi.

China na Urusi vimepinga mara kadhaa kwa kutumia kura zao za turufu kupitishwa kwa azimio la kuiwekea Syria vikwazo vya silaha.

Machafuko ya Syria yamebadili taswira tangu mwaka 2013 baad aya makundi ya wapiganaji wa kislamu wenye itikadi kali kukabiliana na waasi na baadae kuunda eneo la kiislamu katika maeneo ya Iraq na Syria wanayoshikilia. Kwa sasa eneo hilo linaongozwa na Khalifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.