Pata taarifa kuu

Mahakama moja ya kijeshi nchini Marekani yasikiliza kesi ya Ubakaji dhidi ya Jenerali Jeffrey Sinclair

Kesi ya Jenerali wa Marekani Jeffrey Sinclair anayetuhumiwa ubakaji dhidi ya wanajeshi wake wa kike pamoja na kufanya mapenzi nje ya ndoa, imeanza kusikilizwa tangu jana mbele ya mahakama moja ya kijeshi ya Fort Bragg kaskazini mwa mji wa Caroline.

Jenerali Joffrey Sinclair
Jenerali Joffrey Sinclair
Matangazo ya kibiashara

Jenerali huyo mwenye umri wa miaka 51 ambaye aliwahi kuwa naibu kiongozi wa kanda ya 82 ya jeshi la angani, anatuhumiwa makosa 22 ikiwemo ubakaji na kufanya mapenzi nje ya ndoa pamoja pia na kuonyesha mwenendo usio faa katika jeshi.

Iwapo atakutikana na makosa, atafungwa kifungo cha maisha jela. Anashukiwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi kwa kipindi cha miaka mitatu na mtu mwenye umri wa miaka 17 wakati wa kupelekwa majeshi Iraq na Afghanistan, tabia ambayo inapingwa vikali na sheria ya kijeshi nchini Marekani.

Mwanamke huyo ambaye anacheo cha Kepteni anamtuhumu pia ubakaji na kitisho cha kumuuawa yeye na familia yake.

Jenerali huyo amekiri kosa na kufanya mapenzi nje ya ndoa yake. Anatuhumiwa kutumia madaraka yake ya kijeshi katika kutekeleza vitendo vilivyo nje kabisa ya sheria za jeshi la Marekani hususan ubakaji.

Ni nadara sana mahakama ya kijeshi nchini Marekani kusikiliza kesi dhidi ya maafisa waandamizi lakini jeshi la Marekani kutokana na kukabiliwa na katika miezi ya hivi karibuni na ongezeko la matatizo ya kitabia miongoni mwa baadhi ya majenerali, hivyo hakuna budi kusikilizwa kwa kesi hizo.

Mwezi Septemba, Naibu kamanda wa vikosi vya nyuklia, Admiral Tim Giardina alifukuzwa kazi kwa baada ya kutumia kadi bandia katika casino mjini Iowa
Mwaka 2012, General William "Kip" Ward, kamanda wa zamani wa Marekani barani Afrika, alivuliwa cheo baada ya na kutakiwa kulipa $ 82,000 kwa kutumia vibaya kitita cha pesa kilichowekwa kwa ajili ya uongozi wa Pentagon katika harakati zake barani Afrika.

General David Petraeus ambaye hata hivyo hajaadhibiwa lakini alilazimika kujiuzulu kwenye uongozi wa idara ya Ujasusi CIA baada ya kukiri kujihusisha na vitendo vya ngono nje ya ndoa. Kesi utadumu hadi Machi 28.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.