Pata taarifa kuu
COLOMBIA-FARC

Serikali ya Colombia na waasi wa FARC waahirisha mazungumzo ya amani

Serikali ya Colombia na kundi la waasi la FARC kwa pamoja wameahirisha kufanya mazungumzo ya kuleta amani sababu kubwa ikielezwa kuwa wanataka kushirikisha asasi za kiraia katika mchakato huo.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yao pande hizo mbili zimesema kuwa mkutano wao uliokuwa ufanyike kesho utafanyika jumatatu juma lijalo baaada ya kuhakikisha kuwa wawakilishi kutoka kwa raia wa Colombia.

Mkutano huo utafanyika mjii Havanna nchini Cuba , ambapo ajenda kuu tatu zitajadiliwa katika mazungumzo hayo.

Mazungumzo haya yatagusia masuala ya ardhi, ushirikishwaji kwenye maswala ya siasa, ukomeshwaji wa biashara ya dawa za kulevya na kulipa fidia kwa waathirika.

Wakati huohuo waendesha mashtaka nchini Marekani wametoa wito wa kuamuru adhabu ya kifo dhidi ya Mwanajeshi mmoja wa Marekani anayeshutumiwa kuwaua wanakijiji 16 nchini Afghanistan.

Waendesha mashtaka wamedai kuwa kutokana na misingi kuwa mauaji hayo yaliyofanyika mwezi March ni ya kinyama wametaka kesi hiyo kupelekwa kwenye mahakama ya kijeshi.

Sajenti Robert Bales anakabiliwa na mashtaka 16 ya mauaji, majaribio sita ya mauaji na makosa mengine 7 kati ya hayo mawili ya matumizi ya dawa za kulevya na moja matumizi ya kilevi.

Bales mwenye miaka 39 kwa makusudi alitoka katika kambi ya kijeshi iliyo kusini mwa jimbo la kandahar usiku wa March 11 na kutekeleza mauaji dhidi ya wanakijiji wakiwemo watoto 9, na baadae aliichoma moto miili kadhaa baada ya kutekeleza mauaji hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.