Pata taarifa kuu
Marekani

Barrack Obama atangaza mpango wa kubana matumizi ya Jeshi

Rais wa Marekani Barack Obama ametangaza mpango wa kupunguza matumizi ya Jeshi la nchi hiyo linalokabiliwa na kitisho kutoka kwa China huku akisisitiza wataendelea kuwekeza kwenye eneo la asia na Pasifiki.

Rais wa Marekani Barrack Obama
Rais wa Marekani Barrack Obama
Matangazo ya kibiashara

Marekani ambayo ndiyo nchi inayoongozwa kwa kuwa na bajeti kubwa kwenye Jeshi inayofika dola bilioni mia sita na sitini mbili inalazimika kupunguza matumizi yake katika kipindi cha miaka kumi.

Rais Obama amesema hatua hiyo ya kupunguza bajeti haitofanya nchi hiyo kushindwa kupambana na vitisho vyovyote ambavyo vitatokea duniani halikadhalika haitateteresha ushirika na marafiki zake wakiwemo majeshi ya NATO.

Waziri wa ulinzi, Leon Panetta amesema kutakuwa na jeshi dogo madhubuti ambalo litafanya kazi barani Asia na jingine huko mashariki ya kati.

Kwa mujibu wa mpango huo,jeshi hilo litafanya kazi na washirika kutoka Mashariki ya kati ili kulinda usalama katika Ghuba na kuzuia mpango wa silaha za Nuklia wa Iran.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.