Pata taarifa kuu
Marekani

Rais Barrack Obama kutangaza mpango wa ajira

Rais wa Marekani Barack Hussein Obama amewakashfu viongozi wa Chama cha Republican kwa kushindwa kufanyakazi yao ipasavyo wakati wapo madarakani na ameahidi serikali yake kuweka mikakati ya kutengeneza ajira zaidi kukabiliana na uhaba uliopo kwa sasa.

REUTERS/Jason Reed
Matangazo ya kibiashara

 

 

Rais Obama ametaka uungwaji mkono kutoka kwa Wabunge wa Republican na Democratic ili aweze kufanikisha mpango wake wakati huu ambapo nchi hiyo inashuhudia mahitaji ya ajira yakifikia asilimia tisa nukta moja.

Kiongozi huyo wa Taifa kinara kicuhumi ambaye anatarajiwa siku ya alhamisi kuanika mipango yake ya kushughulikia tatizo la ajira kwenye Bunge la Congress.

“Tunapambana ili kuwaletea watoto wetu maisha mazuri hapo baadaye”, alisisitiza Rais Barack Obama.

Uchumi wa Marekani umedorora kiasi na tatizo la ajira linazidi kuongezeka na kwa mfano kwa mwezi wote wa Agosti hakuna ajira zozote zilizozalishwa hali inayotoa changamoto kubwa kwa Rais Obama.

Rais Obama alitumia siku ya kazi kuzungumza na wananchi wa Marekani na amewaomba wananchi kuunga mkono mipango yake ya kuzalisha ajira kwa wingi kulingana na mahitaji ya Wamarekani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.