Rais Hugo Chavez kuteta kiti cha urais mwakani licha ya matatizo ya kiafya
Licha ya matatizo ya kiafya yanayomkabili Rais wa Venezuela Hugo Chavez, msaidizi wake amesema wazi kuwa, kiongozi huyo amepania kutetea nafasi yake, katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika, hapo mwakani.
Imechapishwa:
Akihojiwa na luninga ya taifa, waziri wa fedha wa Venezuela Jorge Giordani, ametoa kauli hiyo, wakati Chavez akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa saratani, nchini Cuba.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 56, ameliongoza taifa hilo, kwa miana kumi na miwili, na angependa kuendelea kushika wadhifa huo, kwa miaka mingi zaidi.
Na kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais wa Cuba Fidel Castro, amewafariji raia wa Venezuela na kuwahakikishia kuwa Chavez, anaendelea vema.