Pata taarifa kuu
Marekani

Kimbunga kingine chaua watu Marekani

Watu wasiopungua 30 wamekufa baada ya kimbunga kupiga katika mji wa Joplin ulioko kwenye Jimbo la Missouri nchini Marekani.

Baadhi ya maeneo yaliyowahi kuathiriwa na kimbunga nchini Marekani
Baadhi ya maeneo yaliyowahi kuathiriwa na kimbunga nchini Marekani ® Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mji huo umepigwa vibaya na kimbunga hicho na baadhi ya maeneo yameharibiwa yakiwemo majengo na mifumo ya simu na umeme.

Kufuatia hali hiyo Gavana wa jimbo hilo, Jay Nixon ametangaza hali ya hatari na ametoa onyo kuwa kimbunga kitaendelea kupiga maeneo zaidi na kuwataka raia kuchukua tahadhari.

Mwezi uliopita kimbuka na radi viliua watu takribani 350 na katika jimbo la Alabama na katika majimbo mengine sita ya kusini mwa Marekani.

Hali ya kimbunga imekuwa tishio kwa wakazi wa maeneo mbalimbali nchini Marekani na watu kukosa makazi huku idadi ya vifo ikitarajiwa kuongezeka.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.