Pata taarifa kuu

DRC: Wanadini wanataka msaada wa kimataifa kulinda misitu ya Afrika

Nchini DRC, madhehebu ya kidini yanatoa mwongozo kwa mawaziri zaidi ya sitini wa mazingira ambao wamekuwa wakikutana tangu Jumatatu mjini Kinshasa kwa ajili ya kazi ya maandalizi ya mkutano kuhusu Tabia nchi (COP27).

Timu ya walinzi wa msituni wakitafuta sokwe katika Hifadhi ya Kahuzi Biega Mashariki mwa DRCongo, Machi 30, 2022.
Timu ya walinzi wa msituni wakitafuta sokwe katika Hifadhi ya Kahuzi Biega Mashariki mwa DRCongo, Machi 30, 2022. © RFI/Charlotte Cosset
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa kidini wanaonya dhidi ya ukataji miti, lakini katika kesi ya DRC ambapo mamlaka inathibitisha nia yao ya kutumia rasilimali za misitu, wanaiomba jumuiya ya kimataifa kuwakataza kwa kuwatoza fidia ya kifedha ndani ya mfumo wa mfuko wa Tabia nchi.

Wanadini wanasema kizingiti cha ukataji miti kinaendelea katika bara zima. Kile ambacho wanadini pia wamelaumu, kuwekwa kando katika usimamizi wa masuala ya Tabia nchi.

"Tunataka kuhimiza serikali zilizopo hapa kusitisha zoezi la ukataji miti na uharibifu wa misitu na kuifanya kuwa kipaumbele chao cha vitendo vyao," amesema Askofu Donatien Nshole wa Kanisa Katoliki nchini  DRC. Kuzingatia miundo ya kidini kama washirika. Miundo hii ni hai katika kuhamasisha, kutoa mafunzo na kuhamasisha waumini wote katika miundo yote kama vile familia, parokia, shule, taasisi na vyuo vikuu”.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.