Pata taarifa kuu
AFRIKA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Afrika Kusini yapiga marufuku raia wake kutoka nje

Serikali ya Afrika Kusini imechukua hatua ya kuwataka raia wake kukaa manyumbani kwao kwa muda siku 21. Hatua mabayo imeanza kutumika rasmi usiku wa manane leo Ijumaa.

Soweto moja ya miji ya Afrika Kusini (picha ya kumbukumbu).
Soweto moja ya miji ya Afrika Kusini (picha ya kumbukumbu). © creative commons/Michael Denne
Matangazo ya kibiashara

Watu milioni 60 nchini Afrika Kusini watalazimika kukaa nyumbani kwa siku 21.

Afrika Kusini ina visa 927 vya maambukizi ya virusi vinavyo sababisha ugonjwa hatari wa Covid-19 (Corona), na ni nchi ya kwanza barani Afrika kuwataka raia wake wote kutotoka nje kwa muda wa wiki tatu.

Hatua hizo zilitangazwa Jumatatu jioni na Rais Cyril Ramaphosa, ambaye alisema anataka kuzuia mlipuko wa janga la Covid-19 na kuepuka janga la kiafya.

Ujumbe wa serikali ya Afrika Kusini uko wazi: "Kaeni nyumbani". Baa, mikahawa, maeneo ya starehe, mbuga, makanisa vimefungwa. Hakuna gari inyopaswa kutembea katika mitaa ya nchi hiyo.

Maafisa pekee wanaofanya kazi katika sekta muhimu ndi ambao wanaruhusiwa kwenda kazini: hospitali, maduka ya dawa, maduka makubwa, maduka ya chakula. Watu wanaofanya kazi katika sekta za maji na umeme wanaweza pia kwenda kazi. Wafanya kazi katika sekta ya migodi ya makaa ya mawe, wataendelea kuripoti kazini.

"Ni marufuku mtu kutoka nje, barabarani, kwenda sehemu anakotaka," ameonya Waziri wa Polisi Mbeki Cele. Nimesikia watu wengine wakizungumza juu ya kwenda kuwatembeza mbwa zao, hakuna swala la kutembeza mbwa! Ikiwa ni muhimu sana, unatakiwa kumtembeza karibu na nyumba yako. "

Polisi, ikisaidiwa mkono na jeshi, wametumwa mitaani ili kutekeleza hatua hiyo, ambayo inaweza kuwa ngumu kutekelezwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.