Pata taarifa kuu
AFRIKA-CORONA-AFYA

Afrika yaendelea kukabiliana dhidi ya Covid-19 (Corona)

Ugonjwa wa Corona unaendelea kushika kasi barani Afrika, huku nchi nyingi zikiendelea kuchukuwa hatua kadhaa za kukabiliana na janga hilo, wakati raia wakiendelea kupuuzia baadhi ya hatua.

Visa 2,137 vya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19 vinaripotiwa barani Afrika, ikiwa ni pamoja na vifo 62, dhidi ya visa zaidi ya 404,000 vya maambukizi ya virusi hivyo na zaidi ya vifo 18,000 duniani kote.
Visa 2,137 vya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19 vinaripotiwa barani Afrika, ikiwa ni pamoja na vifo 62, dhidi ya visa zaidi ya 404,000 vya maambukizi ya virusi hivyo na zaidi ya vifo 18,000 duniani kote. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Nchi za Senegal, Cote d'Ivoire, Sierra Leone na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametangaza hali ya dharura, wakati ugonjwa huo hatari unaendelea kushika kasi katika bara hilo, ambalo raia wake wengi wanakabiliwa na hali duni ya kimaisha.

Kutokana na hali hiyo nchi nyingi za Afrika, hususan Afrika Kusini, zimewataka raia wao kusalia majumbani kwao.

Visa 2,137 vya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19 vinaripotiwa barani Afrika, ikiwa ni pamoja na vifo 62, dhidi ya visa zaidi ya 404,000 vya maambukizi ya virusi hivyo na zaidi ya vifo 18,000 duniani kote, kulingana na tathmini iliyotolewa na shirika la habari la AFP kutoka vyanzo rasmi Jumanne saa 7:00 usiku (sawa na saa tatu usiku saa za Afrika ya Kati).

Hata hivyo udhaifu wa mifumo ya afya ya nchi za Kiafrika huongeza hofu kubwa.

Jumanne wiki hii Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian alitangaza kuwa "msaada wa kifedha" utatolewa kusaidia nchi zilizo hatarini zaidi, hasa nchi za Kiafrika.

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, ameomba nchi zilizostawi kiuchumi na kiviwanda (G20) kusaidia uchumi wa Afrika kwa kuzipunguza mzigo wa madeni na kuandaa mpango wa msaada wa kifedha wa dola bilioni 150.

Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Uchumi barani Afrika, taasisi ya Jumuiya ya nchi za Kiarabu, yenye makao yake Khartoum, imetangaza kwamba inatoa dola milioni 100 kusaidia ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara kukabiliana na janga la Covid-19 (Corona).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.