Pata taarifa kuu
MAREKANI-CALIFORNIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: California yawataka raia wake kusalia nyumbani

Serikali ya Jimbo la California imechukuwa hatua mpya ikiagiza raia wake wakae nyumbani wakati Washington ikiwataka Wamarekani kurudi nchini au kuendelea kubaki nje ya nchi hadi itakapochukiliwa hatua mpya.

Ndege iliyokodiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ili kuwahamisha wafanyakazi wa serikali na Wamarekani wengine kutoka mji wa Wuhan ilipowasili huko Riverside, California.
Ndege iliyokodiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ili kuwahamisha wafanyakazi wa serikali na Wamarekani wengine kutoka mji wa Wuhan ilipowasili huko Riverside, California. REUTERS/Mike Blake
Matangazo ya kibiashara

Idadi rasmi ya watu waliofariki dunia nchini Marekani kutokana na janga la Covid-19 imefikia 200.

Wakati huo huo Marekani inapanga kuchukuwa hatua mpya kwa raia wake wanaosafiri, hasa kwenye mpaka wake na Mexico kama walivyofanya kwenye mpaka na Canada Jumatano wiki hii.

Mamlaka huko California inahofia kwamba zaidi ya nusu ya wakaazi wa jimbo hilo wataambukizwa virusi vya Ugonjwa aw Covid-19 ndani ya kipindi cha wiki nane.

"Tuna hakika kuwa wakazi wa California watatii ( hatua za kukaa nyumbani)," Gavana wa Jimbo la California, Gavin Newsom amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Ametetea maamuzi yake kutokana na utabiri wa kutisha uliotolewa na wataalam ambao wamekadiriwa kuwa asilimia 56 ya wakaazi wa jimbo hilo wanaweza kuambukiwza virusi vya ugonjwa wa Covid-19 ikiwa hakutachukuliwa hatua kali.

Zaidi ya kesi 1,000 za maambukizi zimethibitishwa katika jimbo hilo na watu 18 wamefariki dunia.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.