Pata taarifa kuu
RWANDA-CORONA-AFYA

Rwanda imeanzisha kampeni dhidi ya Corona katika kambi mbalimbali za wakimbizi

Wakati visa vya ugonjwa wa Covid 19 vikiendelea kuongezeka nchini Rwanda ambapo hadi sasa taifa hilo limeripoti visa 11 vya watu wenye virusi vya ugonjwa huo.

Kambi ya Mahama Kusini-mashariki mwa Rwanda, inaohifadhi wakimbizi kutoka Burundi.
Kambi ya Mahama Kusini-mashariki mwa Rwanda, inaohifadhi wakimbizi kutoka Burundi. Philip Kleinfeld
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Rwanda imeanzisha kampeni ya usafi kwenye kambi mbalimbali za wakimbizi nchini humo kwa lengo la kuwalinda wakimbizi waliokimbilia Rwanda kutoambukizwa na virusi vya Corona.

Kampeni hiyo itahusu kambi mbalimbali za wakimbizi ikiwa ni pamoja na kambi ya wakimbizi kutoka DRC ya Kigeme ambayo inapatikana wilayani Nyamagabe, Kusini mwa Rwanda.

Wakimbizi katika kambi hiyo wametakiwa kufuata ushauri wa wizara ya Afya, unaowataka watu wote nchini Rwanda kufuata kanuni za afya ili kujilinda na maambukizi ya virusi vya Corona.

Baadhi ya wakimbizi wamefurahishwa na huduma hiyo ya kuwakumbusha watu kufanya usafi.

“Sio kwamba kila mtu anajua kusoma, kwa hiyo matangazo yanapotolewa kwa njia ya sauti inasaidia kufikisha ujumbe kwa wanaojua kusoma na wasiojua kusoma, tena hufika haraka. ujumbe huo unatusaidia sana kwani unatukumbusha kunawa mikono kila mara, unatukumbusha kuwa mbali na mwenzako pamoja na kutosalimiana, 3 mmoja wa wakimbizi kutoka DRC amesema alipokuwa akihojiwa na mwandishi wetu Kigali Bonaventure Cyubahiro.

Dkt Ganishuli Vedaste anayehudumu katika kituo cha afya katika kambi ya wakimbizi wa DRC ya Kigeme, amesema katika jitihada za kupambana na ugonjwa wa Corona, huwa wanapita nyumba hadi nyumba, wakitoa elimu kuhusu ugonjwa huo.

“Kila mtaa katika kambi una washauri wa afya na wote tumewapa semina kuhusu ugonjwa huo. Wanapita nyumba hadi nyumba wakitoa elimu kuhusu virusi vya Corona” , Amesema Dkt Ganishuli Vedaste.

Mkuu wa kambi hiyoUwambayikirezi Rosete, amesema wakimbizi wamepata mwamko mkubwa juu ya ugonjwa huo na wanafuata ushauri uliotolewa na wizara ya afya nchini Rwanda, MINISANTE.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.