Pata taarifa kuu
UFARANSA-CORONA-AFYA

Wabunge wengine wawili wapatikana na virusi vya Covid-19 Ufaransa

Kesi mbili mpya za maambikizi ya Covid-19 zimeripotiwa miongoni mwa wabunge wa Bunge la Ufaransa, na kupelekea idadi ya wabunge wanne walioambukizwa virusi hivyo. Majina ya wabunge hao hayakutajwa.

Waziri wa Afya wa Ufaransa, Olivier Véran, wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya kikao cha Baraza la Ulinzi na Rais Emmanuel Macron kwenye Ikulu ya Élysée, Machi 8, 2020.
Waziri wa Afya wa Ufaransa, Olivier Véran, wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya kikao cha Baraza la Ulinzi na Rais Emmanuel Macron kwenye Ikulu ya Élysée, Machi 8, 2020. REUTERS/Pascal Rossignol
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo serikali ya Ufaransa imepiga marufuku mikusanyiko ya watu zaidi ya 1,000 katika kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo hatari, Waziri wa Afya, Olivier Véran, alitangaza Jumapili jioni Machi 8, 2020, baada ya kikao cha Baraza la Ulinzi katika ukulu ya Élysée kilichodumu zaidi ya saa mbili.

"Katuka ngazi ya kitaifa, mikusanyiko ya aina yoyote ya watu zaidi ya 1,000 sasa imepigwa marufuku. Mameya, wizara mbalimbali zitaleta orodha ya matukio yanayochukuliwa kama muhimu kwa taifa, Waziri wa Afya, Olivier Véran alitangaz. Maandamano, mitihani na shughuli katika sekta ya usafiri wa umma hazilengwi na marufuku hiyo shirika la Habari laAFP limeripoti.

Tangazo hili litaathiri ulimwengu wa michezo na burudani. Mamlaka tayari imendelea kupiga marufuku matukio mbalimbali kama "Salon du Livre", tukio lililopangwawa kufanyika Machi 20 hadi 23 na tukio jingine muhimu lililopangwa kufanyika Machi 13 hadi 15 huko Paris. Kufikia sasa, mikusanyiko tu ya zaidi ya watu 5,000 ilikuwa imepigwa marufuku hadi katikati mwa mwezi Aprili.

Matukio kadhaa ya michezo yaliahirishwa mwishoni mwa wiki hii iliyopita, pamoja na mchezo wa mpira wa miguu wa Ligi Kuu "Ligue 1" ambao ungelizikutanisha timu za Strasbourg na PSG. Mchezo ambao ungelipigwa Jumamosi, Machi 7.

Kulingana na ripoti iliyotolewa Jumapili saa tisa Alaasiri na idara ya Afya ya Umma nchini Ufaransa, watu 1,126 wameambukizwa virusi vya Covid-19 nchini Ufaransa na kusababisha vifo 16.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.