Pata taarifa kuu

Kiwango cha ukosefu wa ajira chaongezeka hadi 32.9% nchini Afrika Kusini

Kiwango cha ukosefu wa ajira kimepanda katika robo ya kwanza ya mwaka nchini Afrika Kusini, ishara inayotia wasiwasi kwa serikali wiki chache kabla ya uchaguzi wenye ushindani mkubwa tangu miongo kadhaa.

Ukosefu mkubwa wa ajira ni mada kuu katika siasa nchini Afrika Kusini, ambapo Uchaguzi Mkuu utafanyika Mei 29.
Ukosefu mkubwa wa ajira ni mada kuu katika siasa nchini Afrika Kusini, ambapo Uchaguzi Mkuu utafanyika Mei 29. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kiwango cha ukosefu wa ajira kimefikia 32.9% kuanzia Januari hadi Machi, hadi asilimia 0.8 kutoka robo ya awali, kulingana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, StatsSA. "Idadi ya watu wasio na ajira imeongezeka kwa 330,000 hadi milioni 8.2," StatsSA imesema.

Ukosefu mkubwa wa ajira ni mada kuu katika siasa nchini Afrika Kusini, ambapo uchaguzi mkuu na wa serikali za mitaa utafanyika Mei 29. Vijana hasa wanalalamikia ukosefu wa matarajio katika kile ambacho kwa ujumla kinachukuliwa kuwa uchumi wa kiviwanda barani Afrika. Ukosefu wa ajira kwa vijana ulifikia 45.5% katika robo ya kwanza, hadi asilimia 1.3 kutoka kwa robo ya awali.

Kikiwa madarakani tangu ujio wa demokrasia mwaka 1994, Chama cha African National Congress (ANC) kimepoteza baadhi ya uungwaji mkono wake maarufu. Kwa kuzidiwa na kashfa za ufisadi na migawanyiko, chama hicho kitashuka hadi chini ya 50% ya kura kwa mara ya kwanza katika uchaguzi mkuu wa Mei 29, kulingana na kura za maoni. Ikiwa ANC itashindwa kupata wingi wa wabunge, italazimika kutafuta washirika ili kuweka pamoja muungano unaotawala ikiwa inataka kusalia madarakani.

Ukosefu mkubwa wa ajira umesababisha maandamano na chuki dhidi ya wageni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.